Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Valero Texas Open
US PGA Tour
TPC San Antonio
AT&T Oaks Course
San Antonio, Texas, USA
31 March - 3 April 2022
Jordan Spieth anapania kutetea taji la shindano la gofu la
Valero Texas Open kwa mafanikio kule TPC San Antonio na kujiunga na wachezaji wakubwa wa gofu.
Mchezaji huyo raia wa Marekani alishinda shindano hilo mwaka jana kwa kumpiku Charley Hoffman baada ya siku 1,351 bila ushindi.
Akifanikiwa kushinda shindano la mwaka huu, Spieth atajiunga na Bill Mehlhorn, Zach Johnson na Justin Leonard, ambao wamefanikiwa kushinda taji hilo mfululizo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Spieth pia anatazamia kuwa mshindi wa kwanza kushinda Valero Texas Open mara mbili mfululizo tangu Johnson kupata mafanikio hayo mwaka 2008 na 2009.
"Mwaka jana ulikuwa wa kufana sana kwangu na kwa familia yangu baada ya kushinda Valero Texas Open,” Spieth ambaye ni mshindi mara tatu wa Majors bingwa wa kombe FedEx mwaka 2015 alisema.
“Tunatazamia sana kurudi San Antonio na kutetea taji langu. Inafurahisha zaidi kwa sababu itakuwa ni maadhimisho ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa mashindano haya.”
Mabingwa wote nane watakaoudhuria maadhimisho hayo ya miaka mia moja ya Valero Texas Open wameshinda taji hilo ndani ya miaka kumi iliyopita.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Spieth anaungana na Corey Conners (2019), Andrew Landry (2018), Kevin Chappell (2017), Charley Hoffman (2016), Jimmy Walker (2015), Martin Laird (2013) na Brendan Steele (2011).
“Tunapojiandaa kwa makala haya ya kihistoria ya Valero Texas Open, tuna furaha kuwakaribisha mabingwa hawa wa muongo uliopita,” alisema Larson Segerdahl ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Valero Texas Open.
“Tunayo furaha kuwakaribisha wachezaji bora wa gofu duniani ili kusherehekea miaka mia moja ya shindano hili pamoja na jamii ya San Antonio, huku tukikusanya pesa kwa ajili ya kuwasaidia walio na mahitaji.”
Arnold Palmer na Justin Leonard ndio wachezaji wenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano ya gofu ya Valero Texas Open, huku wakishinda mara tatu kila mmoja.
Washindi watano wa mwisho wa Valero Texas Open
2016 - Charley Hoffman - Marekani
2017 - Kevin Chappell - Marekani
2018 - Andrew Landry - Marekani
2019 - Corey Conners - Canada
2021 - Jordan Spieth - Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.