Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 33
Real Sociedad v FC Barcelona
Reale Arena
Donostia-San Sebastián, Spain
Thursday, 21 April 2022
Kick-off is at 22h30
Real Sociedad wanapania kukatisha msururu wa matokeo mazuri ya Barcelona watakapokutana kwenye
mechi ya ligi mnamo Aprili 21 ugani Reale Arena.
Mabingwa hawa wawili wa La liga watakutana kwa mara ya 57 katika mashindano yote tangu msimu wa 1993/94.
Barcelona wameonyesha ubabe kila timu hizi zinapokutana kwani wameshinda mara 37 dhidi ya 8 kwa faida ya Sociedad huku mechi 11 zikiishia sare.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika ligi ilikuwa Agosti 15 2021 ugani Camp Nou ambapo Barcelona iliibuka na ushindi wa 4-2.
Vile vile, Barcelona hawajapoteza katika mechi 11 za ligi zilizopita dhidi ya Sociedad huku wakishinda mechi tisa na kupata sare mbili.
Kwingineko, Sociedad walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya RCD Espanyol kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Aprili 4.
Sociedad hawajapoteza mchezo wa ligi katika michezo sita ya mwisho wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi mara tano na sare moja.
Barcelona wakiwa ugenini walipambana kutoka nyuma na kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya UD Levante kwenye mechi ya Aprili 10.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Huu ilikuwa ni mchezo wa 12 ugenini kwa Barcelona bila kupoteza ikiwa wameandikisha ushindi mara saba na kupata sare tano.
“Levante wanacheza vizuri sana na inahuzunisha kuona wakiwa katika nafasi za kushushwa daraja. Walishinda dhidi ya Atletico na Villarreal,” kocha wa Barcelona Xavi Hernandez alisema.
“Bado tunayo nafasi ya kuimarika japokuwa tunacheza vizuri. La muhimu ni kujiweka vizuri kiakili kuwa tunaweza kupata mafanikio ifikapo mwisho. Tumeonyesha kuwa tunaweza kupata matokeo mazuri hata wakati hatuna mchezo mzuri. Najivunia hawa wachezaji.
“Hatukucheza mchezo mzuri lakini tulijituma sana na mwishowe tukapata alama tatu muhimu. Ter Stegen na Luuk de Jong walitusaidia sana.”
Takwimu baina ya timu hizi, michezo 5 iliyopita ya ligi.
Mechi - 5
Sociedad - 0
Barcelona - 4
Sare - 1
Ratiba ya La Liga mchezo wa 33
Aprili 19 Jumanne
8:00pm- Real Mallorca v Deportivo Alaves
10:00pm- Real Betis v Elche CF
10:30pm- Villarreal CF v Valencia CF
Aprili 20 Jumatano.
8:00pm- Atletico Madrid v Granada CF
9:00pm- Celta Vigo v Getafe CF
10:30pm- CA Osasuna v Real Madrid
ApriIi 21 Alhamisi
8:00pm- RCD Espanyol v Rayo Vallecano
8:00pm- UD Levante v Sevilla FC
9:00pm- Cadiz CF v Athletic Bilbao
10:30pm- Real Sociedad v FC Barcelona
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.