Reds wapania kuwazamisha Magpies


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 35

Newcastle United v Liverpool

St James' Park
Newcastle upon Tyne, England
Saturday, 30 April 2022
Kick-off is at 14h30  
 
Liverpool watapania kuwashinikiza zaidi Manchester City kwa ushindi dhidi ya Newcastle ugani St James' Park Jumamosi ya tarehe 30 Aprili.
 
The Reds wanasalia kwenye nafasi ya pili, alama moja nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City baada ya kushinda mechi mbili kwa mpigo dhidi ya United na Everton.
 
Vijana wa Jurgen Klopp wamecheza mechi 14 za ligi bila kupoteza mechi yoyote, ya mwisho ikiwa dhidi ya mahasimu wao wa jadi Everton Jumapili iliyopita.

Jurgen-Klopp-Liverpool-manager.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Klopp alilazimika kufanya mabadiliko ya kiufundi mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwa sare ya sufuri na mabadiliko hayo yalionekana kuzaa matunda.
 
"Tunafahamu jinsi jedwali lilivyo. Ili kupata ushindi ni sharti kufanya mabadiliko na huo ndio ukweli,” alisema mjerumani huyo.
 
"Tulijaribu kila njia kuzuia kwa sababu Anthony Gordon alikuwa anashambulia kwa kasi na hutungemwacha Joel Matip kupambana naye peke yake.
 
"Tulimwagiza Trent Alexander-Arnold kukaa katika nafasi ya kuzuia mashambulizi na tulitaka Fabinho kumsaidia Matip. Tulifahamu chanzo cha mashambulizi yao japokuwa hatukufanikiwa kuzuia kikamilifu.
 
"Kiukweli bila kuchukua maamuzi magumu wakati mwingine huwezi kushinda mechi. Ilikuwa rahisi kufanya mabadiliko leo na tuliimarisha mchezo wetu baada ya mabadiliko hayo.”
 
The Magpies walikwea jedwali la ligi baada kuishinda timu ya mwisho kabisa Norwich 3-0 wikendi iliyopita na sasa wapo katika nafasi ya tisa, nafasi moja mbele ya Leicester.
 
Huu ulikuwa ni ushindi wa nne kwa mpigo kwa timu ya Eddie Howe ambayo inaendelea kuimarika sana chini ya meneja huyo wa zamani wa Bournemouth tangu achukue mikoba ya kuionoa.

Howe aliisifia klabu hiyo kwa ujumla baada ya kuibuka kutoka nyakati ngumu mwanzoni mwa hatamu yake hadi walipofikia sasa.
 
"Ukitazama nyumna na changamoto tulizopitia awali; kushindwa na Cambridge, bao la dakika za mwisho la Watford, hizo zilikuwa nyakati ngumu na tulikuwa mbali sana na tulipo sasa hivi,” alisema.
 
"Ni kutokana na jitihada za wchezaji, wafanyakazi na mashabiki hadi kufika tulipo. Wametupa motisha kubwa mimi na timu yangu.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Newcastle - 0
Liverpool - 3
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/26/2022