Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 English Premier League
Matchday 33
Manchester United v Norwich City
Old Trafford
Manchester, England
Saturday, 16 April 2022
Kick-off is at 17h00
Manchester United wanapania kupata ushindi kwa mara ya tano mfululizo katika
ligi dhidi ya Norwich watakapokutana Jumamosi Aprili 16. Ni katika juhudi ya kuokoa nafasi ya kumaliza nne bora.
Manchester united walipoteza 1-0 mikononi mwa Everton ugani Goodison Park wikendi iliyopita, na sasa wameachwa kwa alama sita na Tottenham waliopo nafasi ya nne.
Vijana wa Ralf Rangnick wamefanikiwa kupata alama tano kati ya kumi na tano na hili limeathiri sana matumaini yao kumaliza katika nafasi za kwanza nne kwenye ligi.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwa sasa, Rangnick amekiri kuwa wanategemea timu zilizopo juu yao kupoteza mechi na alama kwani timu yake haifungi mabao.
"Tunategemea matokeo ya mechi nyingine kwa sababu sisi tumeshindwa kupata mataokeo mazuri. Ikiwa hatutacheza na kupata matokeo mazuri, vile vile hatuwezi kutegemea kufaidika na matokeo ya timu nyingine,” alisema Mjerumani huyo baada ya kushindwa na Everton.
"Cha muhimu sasa hivi kwetu ni mshikamano. Ndilo tunaweza kufanya hili kujiandaa kwa mchezo dhidi ya Norwich.
"Michezo michache iliyopita hatujawa tukifunga wala kutengeza nafasi za kufunga magoli. Wiki nne au tano zilizopita tulikuwa tukifunga na kutengeneza nafasi za kutosha kama tulivyofanya dhidi ya Watford nyumbani. Leo hatukuweza kufanya hivyo.”
The Canaries waliishinda Burnley 2-0 ugani Carrow Road wikendi iliyopita na kukatisha msururu wa mechi nane bila ushindi wowote.
Hata hivyo, Norwich wapo katika nafasi ya mwisho kwenye jedwali la ligi wakiwa na alama 21, ikiwa ni alama 7 chini ya mstari wa kushushwa daraja na zikisalia mechi saba msimu kukamilika.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kocha wa Norwich Dean Smith amekiri kuwa bado wana kibarua kikubwa ili kuepuka kushushwa daraja lakini ushindi uliopita unawapa matumaini ya kuishinda Manchester United.
"Bado tunapambana. Ushindi wa leo ni mkubwa sio kwetu tu, bali pia kwa mashabiki zetu. Ni kazi kubwa iliyopo mbele yetu lakini tutapambana vilivyo,” alisema Smith.
"Tutajikaza ipasavyo. Ni mechi moja na ushindi mmoja. Tunatazamia mchezo wa wiki ijayo.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi
Mechi - 5
Man United - 4
Norwich - 1
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.