Red Devils wanatzamia ushindi mara mbili dhidi ya Gunners


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 34

Arsenal v Manchester United

Emirates Stadium
London, England
Saturday, 23 April 2022
Kick-off is at 14h30 
 
Manchester United wanapania kupata ushindi wa pili wa msimu katika ligi dhidi ya Arsenal watakapokutana Aprili 23 ugani Emirates Stadium, Jumamosi.
 
Katika mechi ya mkondo wa kwanza, The Red Devils walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Arsenal ugani Old Trafford Disemba 2, huku Cristiano Ronaldo akifunga mabao mawili, la pili akifungwa kwa njia ya penalti.
 
Ulikuwa ni ushindi wa kwanza dhidi ya Gunners katika ligi tangu Aprili 2018 ambapo United walipata ushindi wa 2-1 wakiwa nyumbani Old Trafford, ambao ulikuwa ni ushindi wa pili katika ligi msimu huo wa 2017/18.
 
Timu hizi mbili ni kati ya timu tano zinazopambania nafasi ya kumaliza nne bora kwa manufaa ya ligi ya mabingwa msimu ujao. Nafasi ya nne katika ligi kwa sasa inashikiliwa na Tottenham.
 
Vijana wa Mikel Arteta walionyesha kila uwezekano wa kumaliza nne bora kuelekea miezi miwili ya mwisho ya msimu lakini kushindwa katika mechi tatu mfululizo; Crystal Palace (3-0), Brighton (2-1) na Southampton (1-0) kumetia dosari azma hiyo. Kwa sasa wanashikilia nafasi ya sita, alama nne nyuma ya Spurs.

Ralf Rangnick
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Arteta emekiri kuwa wachezaji wake wamekuwa na wakati mgumu kukubali hali yao ya sasa baada ya kucheza vizuri bila mafanikio yoyote dhidi ya Southampton.
 
"Limewaumiza sana kwa sababu hawakuwa na bahati licha ya kucheza vizuri. Hawajapata ushindi waliouhitaji licha ya kucheza vizuri,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Wanaumizwa na jambo hilo. Mpinzani anapokuzidi maarifa unampa pongezi zake. Unajitathmini na kurekebisha palipoenda mrama. Lazima ujiamini.
 
"Ni vigumu sana kuelezea kinachotokea hasa unapocheza vizuri lakini matokeo sio mazuri. Tumekuwa na mchezo mzuri mara nyingini, tofauti na dakika 25 dhidi ya Crystal Palace na kipindi cha kwanza dhidi ya Brighton.”
 
Manchester United waliwapiku Arsenal na kuingia nafasi ya tano baada ya kushindi mechi dhidi ya Norwich 3-2 wikendi ya pasaka huku Ronaldo akifunga hat-trick yake ya 60.


Mikel Arteta
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mlinzi wa United Victor Lindelof alisifu ushindi dhidi ya Norwich na kusema ni muhimu katika azma yao ya kumaliza katika nne bora. Hii inatokea baada ya Tottenham na Arsenal kupoteza mechi zao.
 
"Alama hizi tatu ni muhimu sana ukizingazitia tulipo katika msimu. Matokeo ya Arsenal na Tottenham yametusaidia sana. Ni sharti tuzidi kupambana,” Lindelof aliiambia MUTV.
 
"Tunahitaji kushinda mechi nyingi iwezekanavyo. Ni imani yetu tutamaliza nne bora.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Arsenal - 2
Man United - 1
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/20/2022