Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 RBC Heritage
US PGA Tour
Harbour Town Golf Links
Sea Pines Resort
Hilton Head Island
South Carolina, USA
14-17 April 2022
Shindano la gofu la
RBC Heritage 2022 linitarajiwa kung’oa nanga katika uwanja wa Harbour Town Golf Links kwenye kisiwa cha Hilton Head jimbo la South Carolina Marekani kati ya tarehe 14 na 17 Aprili.
Shindano hili lilichezwa mara ya kwanza miaka 53 iliyopita katika mwaka 1969. Ni shindano la PGA ambalo kwa sasa huchezwa katikati ya mwezi Aprili wiki moja tu baada ya Masters, Augusta Georgia Marekani.
Benki ya Royal ya Canada imekuwa mfadhili wa taji la Heritage tangu mwaka 2012 na ndio maana ya shindano hilo kupewa jina Royal Bank of Canada (RBC) Heritage.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Stewart Cink ndiye bingwa mtetezi wa taji la RBC Heritage baada ya kushinda taji hilo mwaka jana kwa kuwapiku Emiliano Grillo na Harold Varner III.
Shindano la mwaka huu litajumuisha Dustin Johnson, Patrick Cantlay, Shane Lowery, Collin Morikawa, Cameron Smith, Kevin Kisner, na Chad Ramey.
Shindano litakuwa na wachezaji 144 na litachezwa kwa siku nne, likiwa ni shindano la 26 katika ratiba ya msimu wa 2021-22 wa PGA.
Washindi wa zamani wa RBC Heritage Wesley Bryan, Satoshi Kodaira, Davis Love III, C.T. Pan na Webb Simpson watashiriki pia.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Rais wa wakfu wa Heritage Classic Steve Wilmot ameeleza kuwa Harbour Town Golf Links course ipo tayari kuandaa shindano la mwaka huu la RBC Heritage.
“Tunaiangalia sehemu hiyo kwa ukaribu sana. Kumekuwa na mvua na mvua ndogo lakini haina madhara makubwa kwetu” alisema Wilmot.
“Ni wakati mwafaka. Timu nzima inajituma sana kuanzaia asubui mpaka jioni.
"Tunafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha mambo yanaenda kama yalivyopangwa ili kuwa na wakati mzuri wiki ijayo.”
Davis Love III ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika historia ya shindano hili akiwa ameshinda mara tano.
Washindi 5 wa mwisho wa RBC Heritage
2017 - Wesley Bryan - Marekani
2018 - Satoshi Kodaira - Japan
2019 - CT Pan - Taiwan
2020 - Webb Simpson - Marekani
2021 - Stewart Cink - Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.