Milan kuikaribisha Fiorentina


Image copyright: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 35

AC Milan v ACF Fiorentina 

Stadio Giuseppe Meazza 
Milano, Italy 
Sunday, 1 May 2022
Kick-off is at 16h00
 
AC Milan watakuwa wenyeji wa ACF Fiorentina kwenye mechi ya ligi kuu ya Italia ugani Stadio Giuseppe Meazza Mei 1.
 
Wakiwa ugenini, Rossoneri waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya SS Lazio katika mchezo wa ligi uliopita wa tarehe 24 Aprili.
 
Milan walikuwa hawajashindwa katika mechi 12 za ligi zilizopita huku wakiandikisha sare tano na ushindi mara 7.

Stefano Pioli
Image copyright: Getty Images
 
 
Vile vile, Rossoneri hawajashindwa katika mechi sita za mwisho za ligi wakiwa nyumbani, wakiandikisha ushindi mara tatu na sare tatu ugani Stadio Giuseppe Meazza. 
 
"Najivunia sana wachezaji wangu. Nisingekuwa na furaha kama ningekuwa katika hali yao,” Stefano Pioli, meneja wa Milan alisema baada ya ushindi dhidi ya Lazio.
 
"Wanafaa kupewa heshima yao ambayo kwa muda murefu hawajapata. Kwa miaka mingi sasa wamekuwa wakicheza katika kiwango cha juu kabisa. Tutajitahidi kushinda mechi zote zilizosalia. 
 
Kuna uwezekano hilo halitawezekana lakini tutajituma tuwezavyo. Ratiba iliyosalia sio rahisi na hilo tunalifahamu. Tutaenda hatua kwa hatua, mechi baada ya mechi na kujaribu kadri ya uwezo wetu.”

Jonathan Ikone
Image copyright: Getty Images
 
 
Kwingineko, Fiorentina walikosa ushindi mikononi mwa US Salernitana baada ya kupoteza 2-1 ugenini katika mechi ya ligi iliyochezwa mnamo Aprili 24 na wataialika Udinese Calcio Aprili 27.
 
Ushindi wa US Salernitana ulikatisha msururu wa mechi sita bila kushindwa kwa upande wa Fiorentina kwenye ligi huku wakiandikisha sare mbili na kushinda mara nne.
 
Kabla ya kushindwa na US Salernitana, Fiorentina walikuwa hawajashindwa katika mechi mbili zilizopita za ligi huku wakipata ushindi mara moja na sare moja wakiwa ugenini.
 
Milan na Fiorentina walikutana mara ya mwisho katika ligi Novemba 20 2021.
 
Fiorentina walipata ushindi wa 4-3 dhidi ya Milan katika mechi iliyochezewa ugani Stadio Artemio Franchi ambao ulijulikana kama Stadio Giovanni Berta awali kutokana na mfashisti wa Florence Giovanni Berta.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Milan - 2
Fiorentina - 2
Sare - 1
 

Ratiba ya Serie A mchezo wa 35

 
Aprili 30 Jumamosi 
 
4:00pm- Cagliari Calcio v Hellas Verona 
 
4:00pm- SSC Napoli v US Sasssuolo 
 
7:00pm- UC Sampdoria v Genoa CFC
 
9:45pm- Spezia Calcio v SS Lazio  

 
Mei 1 Jumapili
 
1:30pm - Juventus FC v Venezia FC
 
4:00pm- Empoli FC v Torino FC 
 
4:00pm- AC Milan v ACF Fiorentina 
 
7:00pm- Udinese Calcio v Inter Milan 
 
9:45pm- AS Roma v Bologna FC 

 
Mei 2 Jumatatu
 
9:45pm- Atalanta BC v US Salernitana


Fazer apostas desportivas agora é mais fácil com as novas odds e os mercados mais recente para apostas de futebol. Regista-te já e começa a ganhar com a Betway!


 
Para as mais recentes notícias sobre desporto, dicas de aposta e promoções, siga a Betway no FacebookTwitter, e Instagram. Baixa o aplicativo da Betway.
 

Published: 04/26/2022