Mbio za Portuguese Grand Prix 2022 kung’oa nanga


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP Season

Portuguese Grand Prix

Round 5
Algarve International Circuit
Portimão, Portugal 
Sunday, 24 April 2022

Mbio za 2022 Portuguese Grand Prix zitang’oa nanga Portimão ambao ni mji uliopo wilaya ya Faro eneo la Algarve kusini mwa Ureno mnamo Aprili 24.
 
Hizi zitakuwa ni mbio za mzunguko wa tano wa mashindano ya mwaka huu na zitaandaliwa katika mkondo wa kimataifa wa Algarve uliofunguliwa mwaka 2008.
 
Mwaka 2013 mbio za Portuguese Grand Prix zilifutiliwa mbali na badala yake mbio za Americas za nchini Marekani zikaanzishwa, lakini zilirudishwa kwenye ratiba ya msimu wa 2020.
 
Mbio za hivi karibuni za pikipiki za msimu wa 2022 MotoGP zilikuwa United States Grand Prix na ziliandaliwa kwenye mkondo wa the Americas kule Austin mnamo Aprili 10.

Enea Bastianini
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mbio za United States Grand Prix zilishindwa na Enea Bastianini wa Ducati, ukiwa ni ushindi wa pili kwa raia huyo wa Italia wa msimu huu.
 
Mwendeshaji mwenza wa Bastianini Jack Miller alimaliza wa tatu huku mwendeshaji wa Suzuku Alex Rins akichukua nafasi ya pili katika mbio hizo ambazo ni za nne za msimu huu.
 
Bastianini anaongoza katika jedwali la waendeshaji pikipiki la mwaka 2022 akiwa na alama 61 na anatazamia kuendeleza ubabe huo katika mbio za Portuguese Grand Prix. 
 
Rins na Aleix Espargaro wanachukua nafasi ya pili na tatu kwa alama 56 na 50 mtawalia katika jedwali kuelekea mbio za wikendi inayokuja.

Alex Rins
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mwendeshaji wa Suzuki rider Joan Mir alifurahishwa na juhudi zake kumaliza katika nafasi ya nne kwenye mbio za United States Grand Prix, na sasa anashikilia nafsi ya nne kwenye jedwali la waendeshaji pikipiki.
 
“Ni faraja kubwa kumaliza katika nafasi ya nne hapa. Inamaanisha kuwa tunazidi kuimarika kwenda mbele,” alisema Mir.
 
"Tulikuwa nyuma na tukapambana zaidi katika sehemu za mwisho za mbio hizo. Hatua kwa hatua nilikuwa na wapita na nilikuwa najihisi vizuri.
 
"Nafurahishwa na jinsi mambo yanavyoenda. Nafasi ya nne sio nzuri sana, bora kumaliza ya tano au ya tatu (kicheko) lakini ni nzuri.”
 
Ducati wanaongoza kwenye jedwali la waundaji pikipiki wakifuatiwa na KTM kisha nafasi ya tatu inatwaliwa na Suzuki.  
 

Matokeo ya Portuguese Grand Prix 2021

Mshindi: Fabio Quartararo - Yamaha 
Nafasi ya pili: Francesco Bagnaia - Ducati
Nafasi ya tatu: Joan Mir - Suzuki 


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 
 

Published: 04/21/2022