Madrid wapania kisasi dhidi ya Espanyol


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 34

Real Madrid v RCD Espanyol 

Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain 
Saturday, 30 April 2022
Kick-off is at 17h15  

Real Madrid wataialika RCD Espanyol katika mechi ya ligi ugani Estadio Santiago Bernabéu Aprili 30.
 
The Whites waliendeleza msururu wa matokeo mazuri kwa kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya CA Osasuna ugenini katika mechi ya ligi ya Aprili 20.
 
Madrid wameandikisha ushindi mara nne mfululizo katika mechi nne za ligi zilizopita.

Eduardo Camavinga
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
The Whites walirudi katika kawaida yao ya kushinda walipoishinda Getafe kwenye mechi yao ya mwisho nyumbani Estadio Santiago Bernabeu. Hii ni baada ya Barcelona kuwashinda wakiwa nyumbani na kukatisha msururu wa mechi 24 bila kushindwa kama wenyeji.

“Ni mchezo mgumu sana dhidi ya Osasuna wakiwa nyumbani. Tulionyesha nidhamu kubwa na kupambana vilivyo ili kupata ushindi na tulifanikiwa,” alisema mlinzi wa Madrid Lucas Vazquez baada ya ushindi dhidi ya Osasuna.
 
“Penalti mbili tulizopata zingetusaidia kuwadhibiti wapinzani lakini tulikosa kufunga kwa bahati mbaya japokuwa tulipata ushindi ambao ni muhimu kwa azma yetu ya msimu huu. Tunasalia kileleni na tutapambana sana kunyakuwa taji mapema iwezekanavyo.  
 
"Nafurahi nilifunga goli na kuisaidia timu na juu ya yote kupata nafasi ya kucheza. Ilikuwa furaha kubwa.”

Javi Puado
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Espanyol kwa upande mwingine walipoteza mechi 2-1 dhidi ya Rayo Vallecano wakiwa nyumbani. Mechi hiyo ilichezwa Aprili 21. 
 
Espanyol hawajashinda katika mechi mbili za ligi zilizopita huku wakishindwa katika mechi zote mbili.

Vile vile, Espanyol hawajashinda mechi yoyote ya ligi katika mechi sita zilizopita wakiwa ugenini huku wakiandikisha sare mbili na kushindwa mara nne.
 
Madrid na Espanyol walikutana mara ya mwisho katika ligi mnamo Oktoba 3 2021.
 
Espanyol walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Madrid ugani RCDE Stadium, ambao ni uwanja wa kumi kwa ukubwa Uhispania ukiwa na idadi ya viti 40,000.

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za lig.
Mechi - 5 
Madrid - 4
Espanyol - 1
Sare - 0
 

Ratiba ya La Liga mchezo wa 34

 
Aprili 29 Ijumaa
 
10:00pm- Sevilla FC v Cadiz FC

 
Aprili 30 Jumamosi
 
3:00pm- Deportivo Alaves v Villarreal CF
 
5:15pm- Real Madrid v RCD Espanyol
 
7:30pm- Valencia CF v UD Levante
 
10:00pm- Athletic Bilbao v Atletico Madrid 

 
Mei 1 Jumapili 
 
3:00pm- Elche CF v CA Osasuna 
 
5:15pm- Granada CF v Celta Vigo 
 
7:30pm- Rayo Vallecano v Real Sociedad
 
10:00pm- FC Barcelona v Real Mallorca 

 
Mei 2 Jumatatu
 
10:00pm- Getafe CF v Real Betis 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 04/26/2022