Madrid wako tayari kusimamisha Getafe iliyoimarishwa


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 31

Real Madrid v Getafe CF 

Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain 
Saturday, 9 April 2022
Kick-off is at 22h00  

Real Madrid watamwalika Getafe CF Estadio Santiago Bernabéu Aprili 9 katika mechi ya ligi kuu Uhispania, La liga.
 
Katika mechi ya ligi ya tarehe 2 Aprili, Madrid waliibuka na ushindi wa 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Celta Vigo.
 
Kabla ya kukutana na kuishinda Celta Vigo, Madrid walikuwa wamepoteza mchezo wa ligi dhidi ya Barcelona hapo awali, matokeo yaliyovunja msururu wa mechi nane kwa Madrid bila kushindwa.

Thibaut Courtois
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Ushindi huo wa Barcelona ugani Bernabeu ulimaanisha kuwa Madrid walipoteza kwa mara ya kwanza katika mechi 24 nyumbani, huku wakiandikisha ushindi mara 17 na sare 7.
 
"Ushindi huo ulikuwa muhimu sana. Celta ni timu ngumu unapocheza katika uga wao wa nyumbani. Mechi nilizocheza katika uwanja huu zilikuwa ngumu,” alisema mlinzi wa Madrid Thibaut Courtois baada ya ushindi huo.
 
"Niliokoa mipira mingi katika kipindi cha kwanza. Sijui kama tulifaa kushinda. Tulishambulia eneo lao sana na mwishowe tukapata penalti tatu. Zote zilikuwa penalty halali. Celta hucheza mchezo mzuri na wa kasi sana.
 
"Hatukuwashinikiza vya kutosha katika kipindi cha kwanza. Walitumia sana eneo la katikati ya uwanja lakini mwishowe tuliwadhibiti vizuri. Tumepata alama tatu muhimu sana.”


Mauro Arambarri
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwingineko, Getafe wakiwa nyumbani waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Mallorca katika mechi ya ligi iliyopita ya tarehe 2 Aprili.  
 
Kwa sasa, Getafe wameshinda mechi mbili kwa mpigo na kupata sare moja katika mechi tatu za ligi zilizopita.

Hata hivyo, hawajashinda katika 18 zilizopita wakiwa ugenini baada ya kupata sare nane na kushindwa mara kumi.
 
Mchezo wa mwisho wa ligi baina ya Madrid na Getafe ulikuwa Januari 2 2022.
 
Getafe waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Madrid ugani Estadio Coliseum Alfonso Pérez, uliopewa jina hilo kutokana na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uhispania Alfonso Pérez. Perez alizaliwa na kukulia Getafe.
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi 5 za mwisho za La liga

Mechi - 5 
Madrid - 3
Getafe - 1
Sare - 1
 

Ratiba ya La Liga, mchezo wa 31

 
Aprili 8, Ijumaa
 
10:00pm - Sevilla v Granada 

 
Aprili 9, Jumamosi
 
3:00pm- Cadiz CF v Real Betis 
 
5:15pm- Real Mallorca v Atletico Madrid 
 
7:30pm- Villarreal CF v Athletic Bilbao 
 
10:00pm- Real Madrid v Getafe CF

 
Aprili 10, Jumapili
 
3:00pm- CA Osasuna v Deportvo Alaves 
 
5:15pm- RCD Espanyol v Celta Vigo
 
7:30pm- Elche CF v Real Sociedad
 
10:00pm- UD Levante v FC Barcelona

 
Aprili 11, Jumatatu
 
10:00pm- Rayo Vallecano v Valencia CF 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/05/2022