Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 FIA Formula One World Championship
Fourth Round
2022 Emilia Romagna Grand Prix
Imola Circuit
Imola, Italy
Sunday, 24 April 2022
Mbio za langalanga za
Emilia Romagna Grand Prix zimepangiwa kufanyika eneo la mji wa Emilia Romagna lililopo kusini mwa taifa la Italia mnamo Aprili 24.
Huu ni mzunguko wa nne wa msimu wa shirikisho la mbio za magari wa langalanga, FIA 2022 na utafanyika kwenye mkondo wa Imoa.
Mkondo huu ulipewa jina la mwanzilishi wa Ferrari, marehemu Enzo Ferrari na mwanawe Alfredo “Dino” Ferrari ambaye alifariki mwaka 1956 akiwa na umri wa miaka 24. Kabla ya kifo cha Enzo, mkondo huo ulikuwa ukiitwa Autodromo Dino Ferrari.
Mbio za hivi karibuni za msimu huu zilikuwa ni Australian Grand Prix ambazo zilishindwa na Charles Leclerc wa Ferrari Aprili 10.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
George Russell wa Mercedes na Sergio Perez wa Red Bull Racing-RBPT walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia Australia.
Leclerc anazidi kuongoza katika jedwali la madereva la mwaka 2022 akiwa amejizolea alama 71 kwenye mbio za kwanza tatu za msimu huu.
Russell (alama 37) na Carlos Sainz Jr wa Ferrari (alama 33) wapo katika nafasi ya pili na tatu mtawalia huku wakipania kupunguza nafasi kati yao na Leclerc.
Perez (alama 30), Lewis Hamilton wa Mercedes (alama 28) na Max Verstappen (alama 25) wa Red Bull Racing-RBPT wanachukua nafasi ya nne, tano na sita mtawalia katika jedwali.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Siamini kama nipi katika nafasi ya pili. Niliambiwa lakini sikuwaamini,” Russell alisema baada ya Australian Grand Prix.
"Pengine tunachukua nafasi ya tano kwa timu yenye kasi nyuma ya McLaren na Alphine lakini tupo katika nafasi ya tatu.
"Ni shindano linalotegemea matokeo na sio kasi. Iwapo tunataka kuendelea kubaki katika nafasi hiyo ni sharti tuimarishe gari letu.”
Ferrari wanachukua nafasi ya kwanza katika jedwali la waundaji magari wakifuatiwa na Mercedes na kisha Red Bull Racing-RBPT wanachukua nafasi ya tatu.
Matokeo ya 2021 ya Emilia Romagna Grand Prix
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing-Honda
Nafasi ya Pili: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya tatu: Lando Norris - McLaren-Mercedes
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.