Klabu za Uhispania zina imani kufika hatua ya nusu fainali ya UEFA


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Champions League

Quarter-Final - Second-Leg 

12 and 13 April 2022
Kick-Off 21h00 CAT
 
Real Madrid, Atletico Madrid na Villarreal CF wana imani kufuzu na kuingia hawamu ya nusu fainali ya ligi ya UEFA watakaposhiriki mechi za mkondo wa pili wa robo fainali. 
 
Real Madrid wana imani kubwa kufuzu. Hii ni baada ya kuifunga Chelsea ya England 3-1 Aprili 6 wakiwa ugenini, kabla ya kuwaalika miamba hao wa England ugani Estadio Santiago Bernabeu, Uhispania Aprili 12 kwenye mechi ya marudiano.
 
Madrid wamepoteza mechi moja tu kwenye mechi 15 katika mashindano yote wakiwa nyumbani, na hii ni pamoja na ushindi wa 3-1 dhidi ya PSG ya Ufaransa katika raundi iliyopita ya mechi za UEFA.
 
Iwapo wataepuka kushindwa na Chelsea, Madrid ambao ni mabingwa mara 13 wa mashindano haya watufuzu kuingia nusu fainali.

Unai Emery
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Villarreal watafanya kila wawezalo kuingia nusu fainali kwa kuepuka kushindwa na Bayern Munich, Allianz Arena nchini Ujerumani mnano Aprili 12. Kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya tarehe 6, Villarreal waliishinda Munich 1-0. 
 
Ni kweli Villarreal hawajashinda mechi mbili zilizopita katika mashindano yote wakiwa ugenini lakini wameshinda mechi tatu za mwisho za UEFA wakiwa ugenini.
 
Villarreal waliishinda Juventus ya Italia katika mchezo wao wa mwisho wa ugenini katika UEFA na watakuwa wagani wa Bayern Munich katika mchezo ujao. 
 
"Timu yangu ina ushindani mkubwa,” alisema meneja wa Villarreal Unai Emery baada ya ushindi dhidi ya Bayern, na kuweka wazi kuwa wana imani ya kufika hawamu ya nusu fainali. 
 
"Msimu na uliopita, tumeendelea kuweka kumbukumbu za nzuri. Tunaonyesha kwamba tuko tayari kwa jinsi tunavyocheza dhidi ya wapinzani wakubwa. Tunapambana kuingia nusu fainali.” 
 
"Walicheza kwa weledi sana jioni ya leo.” 

Antoine Griezmann
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwengineko, Atletico wanapania kutumia vizuri mazingira ya uwanja wa nyumbani, Estadio Wanda Metropolitano watakapowaalika Manchester City. Hii ni baada ya kupoteza mechi ya mkondo wa kwanza 1-0 ugenini dhidi ya timu hiyo ya England mnamo Aprili 5. 
 
Mabingwa hao wa Uhispania wamekuwa na matokeo mazuri katika mechi nne za nyumbani katika mashindano yote huku wakiandikisha ushindi wa mechi tatu na kupata sare moja. Sare hiyo ilikuwa dhidi ya wapinzani wa jadi wa City, Manchester United.
 
Atletico wanaofahamika kwa mbinu zao za kuzuia na kushtukiza watafanya wawezalo kuwakatisha tamaa City na kupata matokeo yatakayowapeleka hatua ya nusu fainali.
 
Atletico iliwaondoa miamba wa soka Manchester United katika mashindano haya kwenye raundi ya 16.

Jan Vertonghen
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
SL Benfica wanatarajia kupata ushindi mwingine ugenini watakapokutana na Liverpool ugani Anfield, England Aprili 13.  
 
Timu hiyo ya Ureno ilipoteza 3-1 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Liverpool wakiwa nyumbani na wanapania kurekebisha walipokosea.
 
Hata hivyo, Benfica walifikia hatua hii kwa kuiondoa miamba wa soka kutoka Uholanzi Ajax Amsterdam (1-0) ugenini na watahitajika kutafuta ushindi dhidi ya Liverpool kwa mbinu zote ili kufuzu.
 
Benfica wataingia mchezoni wakiwa na imani ya kuishinda Liverpool kwani pia, Inter Milan waliishinda Liverpool katika mchezo wao wa mwisho wa UEFA wakiwa nyumbani, ambao ulikuwa hawamu ya makundi.
 

Ratiba ya mechi za mkondo wa pili za ligi ya mabingwa.

  
Aprili 12 Jumanne
 
Bayern Munich v Villarreal CF 
 
Real Madrid v Chelsea FC

 
Aprili 13 Jumatano
 
Atletico Madrid v Manchester City 
 
Liverpool FC v SL Benfica 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/11/2022