Juventus kuwa mwenyeji wa Bologna


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 33

Juventus FC v Bologna FC 

Allianz Stadium
Torino, Italy 
Saturday, 16 April 2022
Kick-off is at 19h30  
 
Juventus FC watakuwa mwenyeji wa Bologna FC katika mchezo wa ligi kuu ya Italia ugani Allianz Stadium Aprili 16.
 
Kwenye mchezo wa ligi wa Aprili 9, Juventus wakiwa ugenini walitoka nyuma na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Cagliari Calcio.
 
Ushindi huu dhidi ya Cagliari Calcio waliupata baada ya Inter Milan kukatisha msururu wao wa mechi 16 za ligi bila kushindwa katika mechi ya awali.

Massimiliano Allegri
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kushindwa na Inter kulikatisha msururu wa Juventus wa mechi nane za ligi bila kushindwa wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi mara sita na kupata sare mbili.
 
"Cagliari ni wapinzani wagumu sana hasa wakiwa nyumbani. Wana uwezo mkubwa,” alisema meneja wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya ushindi dhidi ya Cagliari.
 
"Ushindi huu wa leo ulikuwa muhimu sana kwetu kujiweka katika nafasi ya nne. Ingekuwa na athari kubwa kama tungeupoteza. Tuliathirika sana kisaikolojia tuliposhindwa na Inter Milan.
 
"Wachezaji wangu leo walicheza vizuri bila kupoteza mpira kiholela na kupata ushindi waliouhitaji. Mwanzoni mwa mchezo hatukuwa imara lakini tukaimarika kadri mchezo ulivyoendelea.”

Marko Arnautovic
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwengineko Bologna walilazimisha sare ya 0-0 wakiwa ugenini dhidi ya AC Milan katika mchezo wa ligi wa Aprili 4 na watawaalika UC Sampdoria Aprili 11.
 
hawajashinda katika mechi tano za shindano hili huku wakiandikisha sare tatu na kushindwa mara mbili.
 
Vile vile, Bologna hawajashinda mechi yoyote katika mechi sita za mwisho wakiwa ugenini huku wakishindwa mara nne na kupata sare mbili.
 
Mchezo wa mwisho wa ligi baina ya Juventus na Bologna ulikuwa mnamo Disemba 18 2021.
 
Juventus walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Bologna katika mechi iliyochezewa ugani Stadio Renato Dall'Ara, ambao ulijulikana Stadio Littoriale awali.
 
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi
Mechi - 5
Juventus - 5
Bologna - 0
Sare - 0

Ratiba ya Serie A mchezo wa 33
 
Nyakati za Afrika ya kati
 
Aprili 15 Ijumaa
 
7:00pm- Spezia Calcio v Inter Milan
 
9:00pm- AC Milan v Genoa CFC 
 
Aprili 16 Jumamosi
 
12:30pm - Cagliari Calcio v US Sassuolo
 
2:30pm- UC Sampdoria v US Salernitana
 
2:30pm- Udinese Calcio v Empoli FC 
 
4:30pm- ACF Fiorentina v Venezia FC 
 
6:30pm- Juventus FC v Bologna FC 
 
2:45pm- SS Lazio v Torino FC 
 
Aprili 18 Jumatatu
 
7:00pm- SSC Napoli v AS Roma 
 
9:00pm- Atalanta BC v Hellas Verona
 

Published: 04/14/2022