Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Italian Serie A
Matchday 31
Inter Milan v Hellas Verona
Stadio Giuseppe Meazza
Milano, Italy
Saturday, 9 April 2022
Kick-off is at 19h00
Inter Milan itapambana na Hellas Verona katika
mechi ya ligi kuu nchini Italia mnamo Aprili 9 ugani Stadio Giuseppe Meazza.
The Big Grass Snake, kama wanavyojulikana Inter Milan, walipata ushindi wa 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya Juventus FC katika mechi ya ligi iliyochezwa Aprili 3.
Inter Milan wameshinda mechi mbili na kupata sare katika mechi mbili kati ya mechi tano za ligi za mwisho walizocheza.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Wakiwa uga wa nyumbani Stadio Giuseppe Meazza, mabingwa watetezi wa Serie A Inter wameshinda mechi moja na kupata sare moja katika mechi mbili zilizopita.
“Tumepiga hatua na tunawafuata kwa ukaribu viongozi wa ligi Milan na Napoli,” alisema meneja wa Inter Milan Simone Inzaghi baada ya timu yake kupata ushindi dhidi ya Juventus.
"Hivi maajuzi tulipoteza alama na lengo letu ni kufidia alama hizo katika mechi zijazo. Hakuna shinikizo lolote kwa sababu tumefanya vizuri zaidi tulivyotarajia. Hata hivyo matarajio yatakuwepo kila wakati katika timu kubwa kama Inter.
"Siwezi kusahau yalisemwa kipindi ya majira ya joto kuhusu timu hii. Safari bado ni ndefu kwetu. Hii ni hatua tu katika safari inayotukaribisha kwa Napoli na Milan.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwingineko, Verona walilazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Empoli FC wakiwa ugenini katika mechi iliyopita ya ligi, mnamo tarehe 20 Machi na watakuwa wenyeji wa Genoa CFC Aprili 4.
The Mastiffs, ukipenda Verona, hawajashinda katika mechi tatu za ligi zilizopita huku wakiandikisha sare mbili na kushindwa katika mechi moja.
Vile vile, Verona hawajashinda katika mechi nne za ligi za mwisho wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare tatu mfululizo na kushindwa katika mechi moja.
Mchuano wa mwisho wa ligi baina ya Inter na Verona ulikuwa Agosti 27 2021.
Inter walishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Verona katika mechi iliyochezewa ugani Stadio Marc'Antonio Bentegodi, ambao ni uwanja wa nane kwa ukubwa nchini Italia.
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi 5 za mwisho za ligi
Mechi - 5
Inter - 4
Verona - 0
Sare - 1
Ratiba ya Serie A, mchezo wa 32
Aprili 9 Jumamosi
16h00 - Empoli FC v Spezia Calcio
19h00 - Inter Milan v Hellas Verona
21h45 - Cagliari Calcio v Juventus FC
Aprili 10 Jumapili
13h30 - Genoa CFC v SS Lazio
16h00 - SSC Napoli v ACF Fiorentina
16h00 - US Sassuolo v Atalanta BC
16h00 - Venezia FC v Udinese Calcio
19h00 - AS Roma v US Salernitana
21h45 - Torino FC v AC Milan
Aprili 11 Jumatatu
21h45 - Bologna FC v UC Sampdoria
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.