Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 FIA Formula One World Championship
2022 Australian Grand Prix
Albert Park Circuit
Melbourne, Australia
Sunday, 10 April 2022
Lewis Hamilton ana imani kuwa ataibuka na taji kwa mara ya tatu katika mbio za
Australian Grand Prix baada ya kushinda taji hilo mwaka 2008 na 2015.
Muingereza huyo alichukua nafasi ya pili kwenye mbio za mwaka 2019 hata baada ya kuibuka na ushindi kwenye mbio hizo, hivyo basi kusawazisha rekodi ya waliomaliza katika nafasi za kwanza, ambayo ilikuwa mara nane.
Hamilton alikuwa wa pili huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na dereva mwenza wa Mercedes Valtteri Bottas kwenye mbio hizo zilizoandaliwa katika mkondo wa Albert Park Circuit.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Katika mbio za Bahrain Grand Prix mnano Machi 20 ambazo zilikuwa ni mbio za kwanza za mwaka 2022, Hamilton alimaliza wa tatu kabla ya kumaliza kwenye nafasi ya 10 mbio za Saudi Arabian Grand Prix Machi 27.
Hamilton alikuwa na kipindi kigumu cha mazoezi ya Saudi Arabian Grand Prix siku ya Ijumaa, kilichofuatiwa na matokeo mabaya ya mbio za kufuzu tangu mwaka 2009.
Dereva wa Red Bull Racing-RBPT Max Verstappen aliibuka na ushindi wa Saudi Arabian Grand Prix huku Charles Leclerc na Carlos Sainz Jr wote wa Ferrari wakimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.
Kuelekea mbio za Australian Grand Prix, Hamilton yupo nafasi ya tano katika jedwali la madereva huku mshindi huyo mara saba wa dunia wa Formula One akitarajia kuibuka na taji la mbio hizo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Kwa sasa hatupambanii nafasi ya juu kwa sababu tuko nyuma sana ya viongozi. Safari yetu bado ni ndefu. Kwa maoni yangu hatujaimarika,” alisema Hamilton baada ya Saudi Arabian Grand Prix.
"Haas alikuwa na kasi sana sikuweza kushindana na kasi yao. Wana nguvu ya ajabu kwa sababu walinipita kama upepo nilipompita Kevin Magnussen awali katika mbio. Kasi yetu bado iko chini.
"kuna mambo kadha wa kadha ya kushughulikia. Nitazungumza na timu nzima. Inaumiza lakini nilipata alama moja angalau. Sisi sote tulipata alama moja kwa faida ya timu.”
Ferrari wakiwa na alama 78 wanaongoza jedwali la kampuni, Mercedes wapo nafasi ya pili na alama 38 huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Red Bull Racing-RBPT na alama 37.
Matokeo ya 2019 Australian Grand Prix
Mshindi: Valtteri Bottas - Mercedes
Nafasi ya pili: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya tatu: Max Verstappen - Red Bull Racing-Honda
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.