Espargaro aingia mbio za Americas na imani kubwa


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 MotoGP World Championship

2022 Grand Prix of the Americas

Circuit of the Americas
Austin, Texas, United States
Sunday, 10 April 2022
 
Aleix Espargaro wa Aprilia anatarajia kuendeleza alipoachia wikendi iliyopita kwa kushinda mbio za pikipiki zitakazoandaliwa katika mkondo wa Americas Jumapili Aprili 10, baada ya kupata ushindi wa kwanza wikendi iliyopita.
 
Raia huyo wa Uhispania alianza mwaka 2022 kwa kishindo kwa kufanya vizuri katika mbio za kufungua msimu za Qatar Grand Prix na Indonesian Grand Prix.

Maverick Vinales
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Msururu wa matokeo mazuri uliendelea kwa Espargaro kwani aliibuka na ushindi kwenye mbio za Argentine Grand Prix, huku akiwa amefuzu katika nafasi ya kwanza na kuandikisha mzunguko wa wa kasi zaidi.
 
Mwendashi huyo mwenye miaka 32 anaongoza shindano hilo kwa alama 45, ikiwa ni alama saba zaidi ya Brad Binder wa Red Bull KTM. Mwaka uliopita, alimaliza katika nafasi ya 12 kwenye jedwali la waendeshaji na kumaliza mara moja katika nafasi za jukwaani.

Brad Binder
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Espargaro anamatumaini kuwa huu ndio mwanzo tu kwani yeye na wenzake wana mengi ya kusaidia timu ya Aprilia baada ya kuipa ushindi kwa mara ya kwanza.
 
"Haitakuwa rahisi lakini tutapambana na wapinzani wetu kushinda mataji. Huo ndio ukweli!” alisema.
 
"Kama nilivyosema awali, tulifaa matokeo haya. Tulijikakamua sana kwa kweli. Mashindano ya mbio za mwaka huu yatakuwa marefu.
 
"Iwapo tutaendelea kufanya vizuri na kuepuka makosa, tutakuwa kwenye nafasi za jukwaani kila wikendi. Nitajaribu kadri ya uwezo wangu!”
 

Matokeo ya Argentine Grand Prix 2022

 
Mshindi: Aleix Espargaro - Aprilia Racing
Nafasi ya pili: Jorge Martin - Pramac Racing
Nafasi ya tatu: Alex Rins - Team Suzuki Ecstar


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 

Published: 04/08/2022