Citizens kupambana Reds katika mechi ya viongozi wa ligi


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 32

Manchester City v Liverpool

Etihad Stadium
Manchester, England
Sunday, 10 April 2022
Kick-off is at 18h30  
 
Hatima ya ligi ya Premier msimu huu inaweza kuamuliwa wakati Manchester City watakutana na Liverpool ugani Etihad Jumapili Aprili 10.
 
Manchester City wanaongoza ligi, mbele ya Liverpool kwa alama moja huku zikisalia mechi nane msimu kukamilika.
 
Hivi maajuzi, City wameonekana kutetereka baada ya kushindwa dhidi ya Tottenham na kupata sare ya 0-0 dhidi ya Crystal Palace.
 
Hata hivyo, City wamerudia mazingira ya ushindi baada ya kuishinda Burnley 2-0 ugani Turf Moor weekend iliyopita.


Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Guardiola amesisitiza kuwa, sharti wachezaji wake wazoee shinikizo la kushinda kila mechi vinginevyo Liverpool watawapiku na kushinda taji la ligi.
 
"Ni sharti shinikizo liwepo kwa hatuna nafasi ya kupoteza mechi yoyote. Tukipoteza taji litakuwa limepotea,” alisema raia huyo wa Uhispania. “Tujifundishe jinsi ya kukabiliana na shinikizo vinginevyo tutakosa taji.”
 
Vijana wa Jurgen Klopp wamekuwa na msururu wa matokeo mazuri, huku matokeo ya 2-0 dhidi ya Watford wikendi iliyopita ikipelekea kuwa mechi kumi za ligi bila kushindwa.
 
Katika msururu huo, Liverpool wamefunga mabao 25 na kuruhusu mabao mawili tu dhidi yao na kupunguza nafasi baina yao na City.


Jurgen Klopp
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Klopp alisherehekea ushindi dhidi ya Watford kwa furaha sana huku akiongeza kuwa ni muhimu timu yake kuendelea kushinda ili kuwa na ndoto ya kutwaa ubingwa wa ligi.
"Hakuna nafasi ya kupoteza mechi yoyote. Furaha yangu haihusiani na kuwa katika nafasi ya kwanza katika ligi. Ilitokana na kushinda mechi na kuwa na alama 72,” alisema mjerumani huyo.
 
"Ni matumaini yetu. Kuwa mabingwa ni sharti tushinde mechi zetu, la sivyo itakuwa vigumu. Mchezo wa ligi unaofuata utakuwa mkali sana. Sio siri.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Man City - 2
Liverpool - 1
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/06/2022