Chelsea na Madrid kutoana kijasho


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Champions League

Quarter-Final - First-Leg 

Chelsea FC v Real Madrid 
Stamford Bridge
London, England 
Wednesday, 6 April 2022
Kick-Off 22h00  
 
Chelsea FC watakutana na Real Madrid kwenye mechi ya UEFA hawamu ya robo fainali mkondo wa kwanza, Aprili 6. 
 
Chelsea walifuzu kuingia robo fainali kwa kuishinda Lille ya Ufaransa mabao 4-1 katika mechi mbili za raundi ya 16.
 
Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa UEFA wamecheza mechi sita za mashindano haya bila kushindwa huku wakiambuliwa ushindi mara tano na sare moja. 

Thomas Tuchel
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
The Blues pia hawajashindwa katika mechi tano za mashindano haya wakiwa nyumbani baada ya kuandikisha ushindi mfululizo katika mechi zote tano. 
 
"Madrid ni timu ngumu kucheza dhidi. Itakuwa ngumu zaidi kucheza mechi ya mkondo wa pili ugani Bernabeu wakiwa na mashabiki wao wakiwashangilia,” alisema Thomas Tuchel, meneja wa Chelsea. 
 
"Mechi hii ni changamoto kubwa kwetu lakini pia itakuwa ya kusisimua. Tunafahamu ni kitu gani cha kutarajia. Itakuwa mechi ngumu. 
 
"Haijalishi kama tutakutana na mpinzani kutoka England, ni mechi ya UEFA na inafurahisha kucheza dhidi ya timu kubwa Ulaya, lakini ni vizuri kuepuka timu za England kwa sababu tunakutana sana kwenye ligi ya nyumbani.” 

David Alaba
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwengineko, Madrid walifuzu kucheza robo fainali kwa kuishinda PSG ya Ufaransa kwa mabao 3-2 baada ya mechi mbili za raundi ya 16. Paris Saint Germain (PSG) 3-2 on aggregate in the Round of 16 tie.
 
Miamba hao wa soka kutoka Uhispania waliishinda PSG katika mechi yao ya mwisho ya UEFA baada ya PSG ya kuvunja msururu wa Madrid wa mechi nne bila kushindwa katika mechi ya mkumbo wa kwanza wa raundi ya 16. 
 
PSG waliishinda Madrid katika mechi ya kwanza na kuvunja msururu wa Madrid wa mechi tatu bila kushindwa wakiwa ugenini, ambapo wameandikisha ushindi kwenye mechi tatu mfululizo za UEFA.
 
Chelsea na Madrid walikutana mara ya mwisho katika mechi ya UEFA mnamo Mei 5 2021.
 
Chelsea walipata ushindi wa 2-0 katika mechi hiyo ya mkondo wa pili ya nusu fainali ugani Stamford Bridge, England. 
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi ya UEFA 

Mechi: 2
Chelsea - 1
Madrid - 0
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/04/2022