Cavs wapania ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya Knicks


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

New York Knicks v Cleveland Cavaliers

2021-22 NBA Regular Season

Saturday 2 April 2022
Madison Square Garden, New York City, New York
Tip-off at 19:00  
 
The Cleveland Cavaliers watapania kuendeleza msururu wao wa matokeo mazuri watakapochuana na New York Knicks katika ukumbi wa Madison Square Garden jioni ya Jumamosi tarehe 2 Aprili.
 
The Cavs wanapigania kumaliza katika sita bora Eastern Conference japokuwa watahitaji kuongeza juhudi zaidi ili kufuzu moja kwa moja na kuingia katika nafasi ya mechi za mchujo.
 
Vijana wa J.B. Bickerstaff wapo katika nafasi ya saba kwa sasa ligi ya Eastern Conference, wakiwa na rekodi ya 42-33 wakiongozwa na Toronto Raptors katika nafasi ya sita na asilimia 0.013 ya ushindi.

Collin Sexton
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Wamekuwa na matokeo mseto hivi maajuzi, huku wakiandikisha ushindi mara nne katika mechi kumi huku ushindi wa 107-101 dhidi ya Orlando Magic ukivunja msururu wa mechi tatu bila kushinda.
 
Darius Garland alikuwa na mchezo mzuri dhidi ya Magic huku akichangia alama 25. Bickerstaff alimsifia sana kwa mchezo alioonyesha akishirikiana na Lauri Markkanen na kusaidia kupatikana kwa alama 12 katika robo ya nne ambapo ushindi ulipatikana.
 
"Darius ana uwezo mkubwa wa kufunga na kuzuia mashambulizi,” alisema kocha mkuu wa Cavaliers. “Ukiangalia vizuri, ushindi hupatikana katika robo ya nne kwenye mechi nyingi. Unahitaji mchezaji wa kiwango cha juu. Darius ni mchezaji huyo kwetu.”
 
The Knicks walio katika nafasi ya 11, wanapambana sana kuingia katika nafasi ya mchujo baada ya kushinda mechi sita katika ya kumi. Nne kati ya hizo wameshinda kwa mpigo.

Derrick Rose
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
RJ Barrett na Alec Burks walichangia alama 28 na 27 mtawalia, vijana wa Tom Thibodeau walipoishinda Chicago Bulls 109-104, New York City Jumanne na kuongeza nafasi ya kuingia mechi za mchujo.
 
"Kikubwa zaidi, tunawapa vijana chipukizi nafasi ya kucheza na kupata uzoefu wanaohitaji sana. Unasalia kuwa katika shindano hadi utakapotolewa,” alisema Thibodeau. “Naitaka timu yangu izidi kupambana hadi mwisho.”
 
The Cavaliers wameshinda mara mbili dhidi ya Knicks msimu huu, japokuwa walishinda kwa alama mbili tu (95-93) mechi ya mwisho iliyochezwa Januari.
 

Takwimu baina ya New York Knicks na Cleveland Cavaliers, NBA

Mechi: 218
Knicks: 116
Cavaliers: 102
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 04/01/2022