Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 MotoGP World Championship
2022 Argentine Grand Prix
Autodromo Termas de Rio Hondo
Termas de Rio Hondo, Argentina
Sunday, 3 April 2022
Bastianini wa Gresini anapania kuendeleza ushindi katika mbio za pikipiki za
Argentine Grand Prix, raundi ya tatu itakapong’oa nanga Jumapili Aprili 3.
Mwendeshaji huyo kutoka Italia hakufurahia mazingira ya unyevu unyevu katika mbio za Indonesian Grand Prix wiki mbili zilizopita, baada ya kuwa na mbio za kufana za Qatar Grand Prix za kufungua msimu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ikiwa ndio mara yake ya kwanza, Bastianini alimaliza katika nafasi ya 11 kwenye jedwali la waendeshaji pikipiki mwaka jana, akafuzu mkondo wa kimataifa wa Mandalika akiwa wa tano lakini akamaliza nafasi ya kumi na moja baada ya mvua kunyesha.
Mwendeshaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anaendelea kuongoza mbio hizo kwa alama 2, mbele ya Brad Binder wa Red Bull KTM ila anaonekana kuteswa na mbio za mazingira ya mvua.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Ni kweli, mbio hizi hazinifurahishi kwa sababu napendelea mazingira yasiyo ya mvua,” alisema Bastianini. “Yote si sawa. Nilianza polepole na kupoteza nafasi nyingi.
"Baada ya mizunguko saba au nane, kasi yangu iliimarika na nikafanikiwa kumarisha nafasi yangu. Nilikuwa katika nafasi ya nane lakini Binder alinipita kwenye kona ya pili.
"Haikuwezekana tena kuingia nafasi ya nane. Naongoza kwa ujumla katika jedwali lakini hilo sio la maana. Nataka kuimarika katika mbio za kwenye mazingira ya mvua.”
Matokeo ya mbio za Indonesian Grand Prix 2022
Mshindi: Miguel Oliveira - Red Bull KTM Factory Racing
Nafasi ya pili: Fabio Quartararo - Monster Energy Yamaha
Nafasi ya tatu: Johann Zarco - Pramac Racing
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni
soka,
motorsport,
mpira wa kikapu,
rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.