UBINGWA WA NGAO YA JAMII WAMPA JEURI ROBERTINHO


Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amesema ubingwa wa Ngao ya Jamii walioupata ni mwanga mzuri kuelekea msimu mpya wa 2023/24 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
 
 
Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati 3-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Fainali uliopigwa juzi Mkwakwani, Tanga.
 
 
Akizungumza  mara baada ya kukamilika kwa dakika 90, Robertinho alisema furaha yake ya kuchukua taji la kwanza tangu aanze kukinoa kikosi cha timu hiyo alipokuja msimu uliopita.
 
 
Alisema ameshinda mataji mbalimbali katika timu alizozifundisha awali ila ndani ya kikosi cha Simba Ngao ya Jamii waliyoipata kwa kuifunga Yanga kwa ndio la kwanza.
 
 
“Haikuwa mechi rahisi kushinda niwapongeze   wachezaji wangu kujituma
hadi mwisho  kufanikisha kile tulichokitarajia, nina furaha kupata taji langu la kwanza hapa, ni jambo kubwa ambalo linatupa dira kuelekea msimu mpya wa mashindano.
 
 
Nimechukua mataji matatu nikiwa Rwanda na matatu nikiwa Uganda lakini kwa hapa Tanzania hili  lakwanza, niwapongeze  wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kwa kufanikisha hili,” alisema Robertinho.
 
 
Aliongeza kuwa licha  ya kundi moja la wachezaji kuwafiti lakini wameonyesha uwezo mzuri na kila mmoja kufanya majukumu yao kwa kufikia malengo ya kufanikisha kutwaa taji hilo.
 
 
Kocha huyo alisema wachezaji wote wamefanya majukumu yao vizuri ikiwemo safu ya ulinzi iliweza kuimarika vizuri  kuzuia mashambulizi kutoka kwa wapinzani wao walikuwa wakifika katika eneo lao.
 
 
Robertinho amewapongeza mashabiki wa Simba kwa kuendelea kuisapoti timu kila inapokuwa na imekuwa chachu kubwa ya wachezaji kujituma uwanjani kuhakikisha tunapata matokeo chanya.
 
 
“Nawapongeza mashabiki wetu, wanaipenda sana timu yao, mara zote wanajitokeza kwa wingi uwanjani kila timu inapokuwa, hili linaongeza hamasa kwa wachezaji,” alisema Robertinho.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 08/18/2023