Hakimiliki ya picha: Soka la Bongo
KOCHA mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amesema anataka kuona wachezaji wake wakicheza mpira mzuri na tayari ameanza anaona muelekeo wa kikosi chake kucheza soka ambalo analitaka kuliona msimu huu.
Simba juzi ilifanikiwa kukusanya alama tatu zingine kwa kuibuka na ushundi wa mabao 2-0 katika mchezo wa pili wa
Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma jiji FC, ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Robertinho alisema wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu wanapewa nafasi na wanaonyesha uwezo mkubwa ambapo wanaingia taratibu kikosini.
Alisema nyota wapya na wale waliokuwepo awali wameweza kutengeneza muunganiko mzuri na kupata muelekeo wa timu yake kucheza soka ambalo analihitaji la ‘Samba Loketo'.
“Nahitaji kuona mpira mzuri, mpira sio ugomvi ni kipaji na Sanaa, napenda zaidi kushambulia zaidi na kucheza mpira mzuri, matarajio yangu muda mfupi naweza kupata muelekeo wa kile ninachokitaka katika kikosi changu.
"Nimefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wangu hasa wale tuliowasajili msimu huu wanaonyesha kiwango bora na kadiri wanavyopata muda wa kucheza aanazidi kuimarika,” alisema Robertinho na aliongeza kuwa;
“Kadri siku zinavyozidi kwenda wachezaji wanazidi kuzoeana, mimi nimetoka Brazili nimecheza soka na sasa ni mwalimu mara zote naamini kwenye soka la kushambulia pamoja na kumiliki mchezo na hicho ndio nataka wachezaji wangu wakifanye,” alisema Robertinho.
Alisema anawapongeza wapinzani wao Dodoma jiji FC kwa kuonyesha soka nzuri na kuweza kuzuia mipango yao katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza kabla ya kuruhusu bao la kwanza.
Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Dodoma jiji FC, Kassim Liyogope alisema wamefeli mipango yao walioingia katika mchezo wao wa juzi na Simba kwa kukubaki kuchapo cha mabao 2-0 .
Alisema mchezo ulikuwa wa ushindani mkubwa hasa dakika 44 ya kipindi cha kwanza, kwa wachezaji wake kufuata maelekezo waliyowapa kulingana na ubora wa Simba.
“Tuliwasoma vizuri Simba ubora wao upo katikati na pembeni, tulijaribu kuwazuia lakini dakika 44 tulifanya makosa ya kimawasiliano na kuruhusu bao la kwanza.
Kipindi cha pili tulibadili mpango wetu na kufanikiwa kufanya mashambulizi lakini mabadiliko ya Simba kuingia kwa Israel (Mwenda) kucheza na Shomari (Kapombe) ambao wote wanakasi wakazuia mashambulizi ambayo tuliyafanya,” alisema Liyogope.
Aliongeza kuwa kitendo cha Robertinho kumuingiza Kibu (Denis) kwenye kasi na kubadilisha mchezo ikaharibu mipango yao na mabeki wake kuruhusu bao la pili na Simba kutengeneza nafasi nyingi.
“Tumecheza na timu kubwa, wachezaji wana uzoefu mkubwa , kabla hujatamani kucheza na Simba lazima uangalia ubora wao uko wapi jambo tulifanikiwa katika kipindi cha kwanza,” alisema kocha huyo na kuamini kuwa wanaenda kufanyia kazi mapungufu yao yaliyojitokeza kwenye mchezo huo.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.