Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023 FA Community Shield
Arsenal FC v Manchester City
Wembley Stadium
London, England
Sunday, 6 August 2023
Kick-off: 18h00
Arsenal FC na Manchester City watamenyana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii 2023, maarufu kama
FA Community Shield ugani Wembley mnamo Agosti 6.
Cha kufahamu kuhusu shindano hili.
Shindano hili la kila mwaka lilianzishwa mwaka 1908 na shirikisho la soka la England, English Football Association au FA.
Hii ni mechi baina ya mabingwa wa ligi ya Premier na washindi wa kombe la FA, huku mechi hii ikiwa ya 101.
Manchester City walishinda mashindano hayo mawili msimu wa 2022/23 hivyo basi wapinzani wao katika mechi ya ngao ya jamii watakuwa ni Arsenal ambao walimaliza katika nafasi pili kwenye ligi.
Wanaopigiwa upatu.
City wanatarajiwa kushinda mechi hiyo baada ya kuonyesha mchezo mzuri na kuibuka na ubingwa wa ligi ya Premier na vile vile ubingwa wa klabu bingwa ulaya msimu uliopita.
Hata hivyo Arsenal wana nafasi ya kushinda mechi hiyo vile vile baada ya kujasili wachezaji mahiri kwenye kikosi chao kama vile Declan Rice na Kai Havertz.
Tuzo
Mshindi wa mechi ngao ya jamii hutuzwa kombe lililotengenezwa na madini ya kilo 4.2 ya fedha iitwayo sterling 925 silver.
Hata hivyo, mwaka 2019 Manchester City na Liverpool waligawana kima cha pauni milioni 1.25 walipokutana kwenye mechi hiyo. Hii ni kwa mujibu wa chapisho la Manchester Evening News.
Nukuu
Arsenal wamekuwa wakifanya maandalizi ya mechi hii na msimu ujao nchini Marekani.
"Ilikuwa changamoto kwa sababu ya kusafiri kwingi na pia vitu tofauti tulivyo lazimika kuvizoea,” meneja wa Arsena Mikel Arteta alisema.
"Nahisi timu hii ilionyesha ukakamavu katika kuzoea hali tofauti ya joto na muda, viwanja tofauti na wapinzani tofauti. Ulikuwa mtihani mzuri na nimeridhika na matokeo yake,” aliongezea.
"Kuna tofauti kubwa kwa sasa nchini Marekani. Mashabiki wetu wameongezeka. Tulitembea miji mitatu Washington DC, New York na sasa tuko hapa LA. Idadi ya mashabiki inazidi kukua. Asante kwa kila mmoja kwa sababu tunajihisi nyumbani tukiwa hapa.”
Mabingwa watano wa mwisho wa Ngao ya Jamii. (Community Shield)
2018 - Manchester City
2019 - Manchester City
2020 - Arsenal FC
2021 - Leicester City
2022 - Liverpool FC
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.