Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 2
Tottenham Hotspur v Manchester United
Tottenham Hotspur Stadium
London, England
Saturday, 19 August 2023
Kick-off is at 18h30
Manchester United watahitaji kuimarisha uchezaji wao iwapo kushinda mechi ya sita mfululizo dhidi ya Tottenham watakapokutana Jumamosi Agosti 19 Tottenham Hotspur Stadium kwenye
mechi ya ligi.
The Red Devils walionyesha mchezo duni katika mechi yao ya ufunguzi ya ligi nyumbani dhidi ya Wolves licha ya Rafael Varane kuwapa ushindi wa goli moja la dakika ya 76.
Andre Onana alimudu nafasi yake kwenye lango vizuri japokuwa alinusurika kuwapa wageni nafasi ya kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti alipomchezea rafu mshambuliaji Sasa Kalajdzic.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Spurs walianza msimu kwa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Brentford ambapo pia walikosa huduma za mshambuliaji Harry Kane aliyehamia Ujerumani na timu ya Bayern Munich. Goli la kusawazisha la mlinzi Emerson Royal katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza lilihakikisha kuwa Ange Postecoglou anaepuka kushindwa katika mechi yake ya kwanza na klabu ya Tottenham.
Tottenham walianza mchezo huo vizuri baada ya mlinzi Cristian Romero kufunga goli la kwanza dakika ya 11 kabla ya Brentford kusawazisha kunako dakika ya 27 kupitia mchezaji Brian Mbeumo na kisha Yoane Wissa kufunga goli la pili katika dakika ya 36.
Tottenham walitengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli katika kipindi cha pili na kumaliza mchezo huo wakiwa na jumla ya mashuti 18 kuelekezwa kwenye lango la wapinzani.
Mason Mount hakuonyesha makali yake katika mchezo wake wa kwanza na United na meneja Erik ten Hag atahitaji mchezaji huyo kujituma na kusaidia timu hiyo zaidi. Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea aligusa mpira mara 30 kwenye mechi dhidi Wolves, ikiwa ni mara chache kabisa kwa mchezaji wa United, na vile vile hakufanikiwa kupiga shuti hata moja kuelekeza golini mwa wapinzani.
Maddison alikuwa na mwanzo mzuri katika klabu ya Tottenham baada ya kutoa pasi iliyopelekea Romero kufunga goli la kwanza huku pia mchezaji huyo wa zamani wa Leicester akitoa pasi sita muhimu kwenye mchezo huo.
Ten Hag alikiri kuwa timu yake ilipoteza mpira kwa wapinzani mara kwa mara japokuwa alifurahishwa na kitendo cha timu hiyo kutokuruhusu goli lolote wakiwa nyumbani, ambapo waliruhusu magoli 10 tu msimu uliopita.
"Tulipoteza mpira kiholela. Hatukufanya vizuri. Ni jambo la kawaida hasa msimu unapoanza lakini tutajitahidi kuimarika,” alisema raia huyo wa Uholanzi.
"Unapopoteza mpira kiholela unampa mpinzani fursa ya kushambulia na utalazimika kumfuata ili kudhibiti shambulizi hili. Nahisi tulifanya hivyo na kuzuia maafa.
"Ni vizuri kutokuruhusu goli hasa tukiwa hapa nyumbani Old Trafford. Tunachotakiwa sasa ni kujiimarisha katika kumiliki na kudhibiti mpira tunapokuwa nao.”
Postecoglou alifurahi kupata alama moja kwenye mechi yake ya kwanza na kuwapongeza wachezaji wake kwa kuwa watulivu walipokuwa chini ya shinikizo katika kipindi cha kwanza.
"Nimefurahishwa na juhudi za wachezaji kwa ujumla. Ni mwanzo mzuri kwetu,” alisema raia huyo kutoka Austria.
"Tulikuwa chini ya shinikizo katika sehemu za kipindi cha kwanza lakini wachezaji hawa walimudu nyakati hizo vilivyo kwa maoni yangu.
"Tulidhibiti mchezo huo vizuri katika kipindi cha pili ila hatukuweza kuzitumia vizuri hasa katika kufunga magoli. Tulikosa ubunifu ila nahisi tulijitahidi sana chini ya hali tuliyokuwepo.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Tottenham - 0
Man United - 4
Sare - 1
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 2:
Majira ya Afrika ya Kati
Ijumaa, Agosti 18
8:45pm: Nottingham Forest v Sheffield United
Jumamosi, Agosti 19
4:00pm: Fulham v Brentford
4:00pm: Liverpool v Bournemouth
4:00pm: Wolverhampton Wanderers v Brighton & Hove Albion
6:30pm: Tottenham Hotspur v Manchester United
9:00pm: Manchester City v Newcastle United
Jumapili, Agosti 20
3:00pm: Aston Villa v Everton
17h30: West Ham United v Chelsea
Jumatatu, Agosti 21
9:00pm: Crystal Palace v Arsenal
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.