EPL - Newcastle United v Liverpool


Alamy hisa picha


2023/24 English Premier League

Matchday 3

Newcastle United v Liverpool

St James' Park

Newcastle upon Tyne, England

Sunday, 27 August 2023

Kick-off is at 18h30 
 

Liverpool wanapania kupata ushindi wao wa pili wa ligi msimu huu watakapokabiliana na Newcastle ugani St James' Park Jumapili, Agosti 27.

 

The Reds walipata alama moja tu kwenye mechi yao ya kwanza ya msimu dhidi ya Chelsea Stamford Bridge baada ya kutoa sare ya 1-1 huku Axel Disasi akisawazisha goli la Luis Diaz.

 

Timu hiyo chini ya Jurgen Klopp ilipata ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya Bournemouth siku sita baadaye ambapo Diaz alifunga tena goli lingine. 

 

Suggested photo: Alexander Isak of Newcastle

 

The Magpies walianza msimu huu kwa mafanikio makubwa walipowagaragaza Aston Villa 5-1 nyumbani huku Alexander Isak akifanikiwa kufunga magoli mawili katika mechi hiyo. 

 

Kwenye mechi iliyofuata, Newcastle walipoteza 1-0 ugenini dhidi ya Manchester City katika mchezo wa kusisimua uliochezewa ugani Etihad.  

 

Meneja wa Newcastle Eddie Howe anatarajia timu yake itajizoa na kuikabili vilivyo Liverpool kwani walifanikiwa mikwaju saba tu kwenye goli la City huku shuti moja tu likilenga golini. 

 

Isak alijituma sana bila mafanikio katika mechi hiyo na mwishowe aliondolewa uwanjani huku nafasi yake ikichukuliwa na Callum Wilson dakika ya 66. Msimu uliopita, mshambuliaji huyo wa Sweden alionyesha mchezo mzuri baada ya kurejea kutoka majeruhi huku akifanikiwa kufunga magoli 10 kutokana na mechi 22 na kumuweka nje ya kikosi cha kwanza Wilson ambaye miezi miwili ya mwisho ya msimu aliimarika zaidi na kumaliza msimu na magoli 18. 

 

Suggested photo: Luis Diaz of Liverpool

 

Diaz alikuwa katika hali nzuri kwenye mechi za maandalizi ya msimu mpya na anaonekana kuendeleza hali hiyo huku akipania kufunga goli katika mechi tatu mfululizo akiwa na Liverpool kwa mara ya kwanza. Msimu wa kwanza na Liverpool kwa raia huyo wa Colombia ulikuwa na changomoto si haba kwa alikosa mechi 21 baada ya kupata jeraha baya la goti na kufanikiwa magoli manne tu. 

 

Howe alikiri walikuwa na uwezo wa kuifunga City japo walijituma na kuzuia maafa zaidi. 

 

"Ulikuwa mchezo mgumu kama tulivyodhani. City ni timu yenye uwezo mkubwa. Tulijaribu sana kutumia mbinu zetu dhidi yao lakini wilidhibiti mipango yetu,” alisema.

 

"Hatukutumia nafasi zetu ilivyofaa tulipozipata. Tulicheza vizuri sana kipindi cha pili. Hatukuwa na uchovu ila tulikosa ufundi. Hatukumiliki mpira ipasavyo. 

 

"Nahisi tulizuia vizuri. Tulishambulia kutoka mwanzo wa mchezo. Hatukusubiri kushambulia kwa kushtukiza. Tulijikita kwenye mbinu zetu ila hatukupata matokeo tuliyoyataka.” 

 

Klopp alisifia juhudi za Diaz dhidi ya the Cherries na ana imani atazidi kuisaidia timu iwapo hatopata matatizo ya afya au majeraha. 

 

"Lucho ni mchezaji wa kiwango cha juu anapokuwa. Halina shaka hilo. Alifunga goli zuri kabisa. Yupo katika hali nzuri kwa sasa ila kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwake vile vile,” alisema Klopp. 

 

"Tulikuwa na mfumo tofauti katika safu ya kati na ilikuwa vigumu kwake kama tulivyoshuhudia. Tofauti na hilo, alionyesha mchezo mzuri kabisa. Ni tishio kwa mpinzani yeyote. Yupo katika hali nzuri kwa sasa.” 

 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Liverpool - 4
Newcastle - 0
Sare - 1

 

Ratiba ya ligi ya Premier mchezo wa 3:

 

Ijumaa, Agosti 25

10:00pm: Chelsea v Luton Town

Jumamosi, Agosti 26

2:30pm: Bournemouth v Tottenham Hotspur

5:00pm: Arsenal v Fulham

5:00pm: Brentford v Crystal Palace

5:00pm: Everton v Wolverhampton Wanderers

5:00pm: Manchester United v Nottingham Forest

7:30pm: Brighton & Hove Albion v West Ham United

Jumapili, Agosti 27

4:00pm: Burnley v Aston Villa
4:00pm: Sheffield United v Manchester City
6:30pm: Newcastle United v Liverpool

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 08/25/2023