Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 1
Burnley v Manchester City
Turf Moor
Burnley, England
Friday, 11 August 2023
Kick-off is at 22h00
Baada ya kurejea kwenye ligi na Burnely, kibarua cha kwanza cha Vincent Kompany kitakuwa dhidi ya waajiri wake wa zamani Manchester City ugani Turf Moor Ijumaa Agosti 11 katika
mechi ya ufunguzi wa ligi.
Kompany alikuwa mchezaji wa City kwa miaka 11 kabla ya kujiunga tena na timu yake ya utotoni Anderlecht mwaka 2019 na baadaye kustaafu baada ya msimu mmoja.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Ubelgiji alirejea tena England mwaka 2022 kuifunza Burnley ambao aliwasaidia kupandishwa daraja katika msimu wake wa kwanza. Hii ni baada ya kuwa mkufunzi kwa miaka miwili kabla wa Anderlecht.
Burnely chini ya Kompany walishinda ligi ya daraja la pili kwa alama 101 na kuwa klabu ya sita katika historia ya ligi hiyo kufikisha alama 100 na ya kwanza tangu Leicester kufanya hivyo msimu 2013-14.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
City walishinda kombe la ligi kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuwabandua Arsenal kileleni, waliodumu siku 248 katika nafasi hiyo kabla ya kuteleza huku zikisalia mechi tano msimu kukamilika.
Vijana wa Pep Guardiola walishinda mechi 16 za ligi mfululizo kabla ya kupoteza mechi ya mwisho 1-0 dhidi ya Brentford siku ya mwisho ya msimu.
Hata hivyo, City walipoteza mechi ya ngao ya jamii (Community Shield) 4-0 dhidi ya Arsenal kwa njia ya matuta ya penalti, mechi ambayo uhashiria mwanzo wa msimu mpya.
Phil Foden alifunga mabao 11 na kuchangia mengine 32 msimu uliopita, ambao kwa kiwango kikubwa ulikuwa msimu wake bora akiwa na timu hiyo. Kocha Guardiola alimsifia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa mchango wake na kusema kuwa atakuwa na nafasi zaidi ya kufanya hivyo msimu ujao wa 2023-24 kufuatia kuondoka kwa Riyad Mahrez.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nathan Redmond amerejea tena England baada ya kutumikia Besiktas ya Uturuki kwa msimu mmoja ambako alifunga magoli matano katika mechi 25 za ligi, yakiwemo magoli matatu dhidi ya Kayserispor, Istanbulspor na Fenerbahce. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alishiriki mechi 232 akiwa na Southampton kwa kipindi cha miaka 7 kabla ya kutimkia Uturuki.
Redmond ni mmoja wa wachezaji tisa waliosajiliwa na Burnley. Hata hivyo Kompany aliashiria kuwa kuna uwezekano wa wachezaji zaidi kusajiliwa kabla ya mwezi Agosti kukamilika huku akiendelea na maandalizi ya msimu unaokuja.
"Muda wote ni muda wa kujiimarisha. Nahisi hili ni jibu utakalopata kwa wakufunzi wote katika ligi,” aliambia Clarets+.
"Kimwili tumejiandaa vilivyo. Kiakili vile vile. Ila tuna mwezi mmoja wa kufanya usajili zaidi na kuimarisha kikosi chetu.”
Guardiola alipata muda wa kuwachezesha Foden, Kevin De Bruyne na mfungaji Cole Palmer ambao hawajashiriki mchezo wowote tangu fainali ya UEFA.
"Ni sharti kukabiliana na hali iliyopo. Tumeonyesha kuwa tuna uwezo huo. Tumeshindana na timu nzuri. Ilitokea msimu jana na imetokea tena msimu huu,” alisema raia huyo wa Uhispania.
"Tulikuwa karibu na ubingwa lakini matokeo hayakwenda upande wetu. Ni jambo la kawaida katika mpira. Hata bila ushindi, wachezaji wamepata nafasi ya kujiweka tayari kwa ajili ya ligi. Kwa sasa nawaza kuhusu mchezo wa Ijumaa dhidi ya Burnley.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Burnley - 0
Man City - 5
Sare - 0
Ratiba ya mechi za Premier, mchezo wa kwanza:
Agosti 11 Ijumaa
10:00pm: Burnley v Manchester City
Agosti 12 Jumamosi
2:30pm: Arsenal v Nottingham Forest
5:00pm: Bournemouth v West Ham United
5:00pm: Brighton & Hove Albion v Luton Town
5:00pm: Everton v Fulham
5:00pm: Sheffield United v Crystal Palace
7:30pm: Newcastle United v Aston Villa
Agosti 13 Jumapili
4:00pm: Brentford v Tottenham Hotspur
6:30pm: Chelsea v Liverpool
Agosti 14 Jumatatu
10:00pm: Manchester United v Wolverhampton Wanderers
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.