Shindano la BMW Championship 2022 kung’oa nanga.


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 BMW Championship 

US PGA Tour 

Wilmington Country Club
Wilmington, Delaware, USA 
18-21 August 2022 
 
Shindano la gofu la BMW Championship mwaka 2022 linatarajiwa kung’oa nanga Wilmington Country Club, Delaware, Marekani kati ya tarehe 18 na 21 Agosti 
 
Shindano hili liliasisiwa mwaka 2007 na shirikisho la gofu la Western Golf Association na lilifahamika kama Western Open.
 
Shindano hili la BMW Championship lilitajwa kuwa shindano la mwaka, mwaka 2012, 2013 na 2014 na PGA Tour. Vile vile, ni shindano la zamani kabisa katika ratiba ya PGA Tour.
 
Shindano hili hushirikisha wachezaji walio katika nafasi za kwanza 70 kwenye PGA Tour. Linafuatiwa na shindano la gofu la FedEx St. Jude Championship ambalo lilishindwa na  Will Zalatoris Agosti 14.
 
Bingwa wa sasa ni Patrick Cantlay ambaye alishinda shindano la mwaka 2021 la BMW Championship na ulikuwa ni ushindi wake wa kwanza wa shindano hili.
 
Miongoni mwa wachezaji katika shindano la mwaka huu ni pamoja na Jon Rahm, Scottie Scheffler, Rory McIlroy pamoja na Cantlay anayetarajiwa kutetea taji lake.
 
Wachezaji wanne; Lucas Glover, Adam Scott, Andrew Putnam na Wyndham Clark walifuzu kuingia 70 bora katika shindano la FedEx St. Jude Championship.
 
Shindano litakuwa na zawadi ya pesa kiasi cha dola milioni 15 za kimarekani huku wachezaji 36 waliopo 50 bora kwenye jedwali rasmi la dunia la gofu wakipigiwa upatu kushinda.
 
Cameron Smith ambaye anashikilia nafasi ya tatu katika shindano la FedExCup amejiondoa kwenye shindano la BMW Championship kutokana jeraha la kiuno.
 
“Kwa bahati mbaya Cam hatoweza kushiriki shindano la BMW Championship wiki hii Wilmington,” alisema Bud Martin ambaye ni wakala wa Smith.
 
“Amekuwa akiuguza jeraha la mara kwa mara la kiuno kwa miezi kadhaa. Amechukua uamuzi wa kupumzika wiki hii.”
 
Tiger Woods na Dustin Johnson ndio wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya shindano la BMW Championship ikiwa wameshinda mara mbili kila mmoja.
 

Mabingwa watano wa mwisho wa shindano la BMW Championship

 
2017 - Marc Leishman - Australia 
2018 - Keegan Bradley - Marekani 
2019 - Justin Thomas - Marekani  
2020 - Jon Rahm - Uhispania 
2021 - Patrick Cantlay - Marekani  
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 
 

Published: 08/17/2022