Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 3
Manchester United v Liverpool
Old Trafford
Manchester, England
Monday, 22 August 2022
Kick-off is at 22h00
Manchester United watakuwa ange kuzuia kichapo kingine mikononi mwa Liverpool watakapokutana ugani Old Trafford Agosti 22 Jumatatu.
Mkufunzi mpya wa United Erik ten Hag ameanza vibaya kazi yake mpya kwa kupoteza
mechi mbili za kwanza za ligi za msimu 2022/23.
United walishindwa na Brighton 2-1 ugani Old Trafford katika mechi ya kwanza ya ligi msimu huu kabla ya kupata kichapo kikali cha 4-0 dhidi ya Brentford Jumamosi.
Mabao yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza, ambayo ni mara ya kwanza kwa United kuruhusu magoli manne dakika za kwanza 36 za mechi tangu ligi hii ilipobadilisha jina na kuitwa Premier league.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ten Hag anajituma sana ili kubadilisha hali hii kwa haraka lakini ameitaka klabu hiyo kusajili wachezaji zaidi baada ya kuwasili kwa Lisandro Martinez, Tyrell Malacia na Christian Eriksen katika dirisha hili la uhamisho.
"Timu yetu inapitia wakati mgumu,” raia huyo wa Uholanzi alikiambia kituo cha runinga cha Skysports baada ya mechi.
Kileleni mwa msimamo na nafasi ya kushinda zawadi bab-kubwa
Chomoka na Odds msimu huu na unaweza kushinda mgao wa mamilioni ya zawadi.
Kuanzia pesa taslimu hadi Free Bets na mzigo wa vifaa vya nyumbani ikiwemo TV, home theatre, jiko na mashine ya kufulia, kuna mechi nyingi za kubashiri kila wiki.
"Tulitarajia mwanzo hautakuwa rahisi. Hali hii inajirudia baada ya msimu uliopita. Ni jukumu letu kubadilisha hali hii haraka iwezekanavyo.
"Tunahitaji wachezaji wapya wazuri na tutafanya kila tuwezalo kuwashawishi waje.”
Kwa upande wao, Liverpool vile vile mwanzo wao haujawa mzuri kwa sababu tayari wapo alama nne nyuma ya viongozi Manchester City baada ya mechi mbili.
Vijana wa Jurgen Klopp walilazimisha sare ya 2-2 dhidi ya timu iliyopandishwa daraja, Fulham kwenye mechi ya kwanza ya msimu huu kabla ya kupata sare nyingine Jumatatu dhidi ya Crystal Palace.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Klopp anapambana na majeraha ya wachezaji kadhaa huku Joel Matip, Roberto Firmino, Thiago Alcantara, Curtis Jones, Alex Oxlade-Chamberlain, Ibrahima Konate, Calvin Ramsay, Diogo Jota na Caoimhin Kelleher wakiuguza majeraha. Vile vile, watakosa huduma za Darwin Nunez aliyeonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Crystal Palace.
"Wiki hii imekuwa ya ajabu. Nimeshuhudia wiki nyingi lakini wiki hii ni kama kulikuwa na mchawi mjengoni,” alisema raia huyo wa Ujerumani kuhusu majeruhi.
"Umekuwa mwanzo mbaya kwetu lakini hali sio nzuri kutokana na wachezaji wengi kuwa majeruhi. Tunangoja kuona ni wangapi watarudi wiki ijayo.
"Darwin amepata kadi nyekundu leo lakini Bobby (Firmino) huenda akarudi wiki ijayo. Hakuna wasiwasi sana kwa sababu ndio mwanzo wa msimu tu.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Man United - 0
Liverpool - 4
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.