Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Tour Championship
US PGA Tour
East Lake Golf Club
Atlanta, Georgia, USA
25-28 August 2022
Jon Rahm anapania kushinda shindano la gofu la
Tour Championship baada ya kukosa taji hilo kwa nafasi ndogo sana mwaka jana.
Mchezaji huyo kutoka Uhispania aliponea kiduchu kushinda shindano hili miezi kumi na mbili iliyopita aliposhindwa na Patrick Cantlay kwenye mechi ya muondoano.
Hakuna mchezaji kutoka Uhispania aliyewai kushinda shindano hili la Tour Championship. Rahm anatarajia kuandika historia mpya kwa shishinda taji hili baada ya kushinda mataji saba ya PGA Tour.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Rahmbo, kama anavyojulikana Rahm kwa mashabiki wake, aliwahi kushikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali rasmi la gofu duniani.
Raia huyo wa Uhispania alishika nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza aliposhinda shindano la gofu la Memorial Tournament mwezi Julai miaka miwili iliyopita. Mwezi Juni mwaka 2021 Rahm aliweka historia kwa kuwa raia wa kwanza kushinda shindano la gofu la US Open.
Mwezi Mei mwaka huu, Rahmbo aliibuka na ushindi wa shindano la Mexico Open 2022.
Huu ni ushindi wa pekee kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika msimu huu wa 2021-22 PGA Tour na ana uchu wa kumaliza msimu kwa ushindi huku akiwa anashikilia nafasi ya 11 kwenye msimamo wa FedEx Cup.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
.
“Lengo langu ni kumaliza katika nafasi ya juu zaidi iwezekanavyo. Nia ya kucheza ni ushindi. Nafasi ya kwanza ikishindikana, nafasi ya pili itanifaa,” alisema Rahm akizungumzia msimamo wake kwenye FedEx Cup wiki moja iliyopita.
"Nafasi ya thelathini ni bora kuliko thelathini na moja. Hakuna mabadiliko ya mtazamo wangu. Nafahamu wazi athari zinaweza kuwa kubwa zaidi kuelekea wiki ijayo kutegemea na uchezaji wako. “
Tiger Woods ndiye mchezaji aliye na mafanikio makubwa katika historia ya Tour Championship ikiwa ameshinda shindano hilo mara tatu.
Washindi watano wa mwisho wa shindano la gofu la Tour Championship
2017 - Xander Schauffele - Marekani
2018 - Tiger Woods - Marekani
2019 - Rory McIlroy - Northern Ireland
2020 - Dustin Johnson - Marekani
2021 - Patrick Cantlay – Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.