Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 MotoGP Season
2022 Austrian Grand Prix
Round 13
Red Bull Ring
Spielberg, Austria
Sunday, 21 August 2022
Mbio za pikipiki za Austrian Grand Prix 2022 ambazo pia zinajulikana kama Motorrad
Grand Prix von Österreich zitang’oa nanga Agosti 21 kule Spielberg.
Hizi zitakuwa mbio za 13 za mashindano ya mwaka huu na zitaandaliwa kwenye mkondo wa Red Bull Ring ambao ulijulikana hapo awali kama Österreichring.
Mwendeshaji wa kampuni ya KTM Brad Binder alishinda mbio za mwaka jana za Austrian MotoGP huku waendeshaji wa Ducati Francesco Bagnaia na Jorge Martin wakimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.
Mbio za hivi karibuni za msimu huu wa 2022 wa MotoGP kuandaliwa zilikuwa za British MotoGP, maarufu kama Monster Energy British Grand Prix na ziliandaliwa mnamo Agosti 7.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Bagnaia alishinda mbio za British MotoGP 2022, ambazo zilikuwa mbio zake za nne kupata ushindi msimu huu baada ya kushinda Dutch MotoGP, Italian MotoGP na Spanish MotoGP awali.
Jack Miller wa Ducati alimaliza katika nafasi ya tatu na nafasi ya nne kutwaliwa na mwendeshaji wa Aprilia Maverick Viñales katika mbio hizo.
Mwendeshaji wa Yamaha Fabio Quartararo anaongoza jedwali la 2022 la waendeshaji baada ya kujizolea alama 180 huku akipania kutetea taji la MotoGP kwa mafanikio.
Aleix Espargaro wa Aprilia na Bagnaia wanashikilia nafasi ya pili na tatu wakiwa na alama 158 na 131 mtawalia.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mshindi wa mwaka jana wa mbio za Austrian MotoGP Brad Binder alimaliza katika nafasi ya 11 katika mbio za British MotoGP, sekunde saba tu nyuma ya mshindi Bagnaia.
“Tulikuwa na kasi nzuri kwenye mbio hizo,” alisema raia huyo wa Afrika kusini aliye katika nafasi ya saba kwenye jedwali la waendeshaji.
"Tulijaribu sana kutumia muda mchache kwa mzunguko katika kufuzu. Nilianza mbio vizuri lakini kwenye mzunguko wa tano nilipata hitilafu kidogo na kupitwa na watu watano.
"Hitilafu hiyo ilipelekea kupoteza nafasi tano mbele yangu. Japokuwa nilifanikiwa kufikia waliokuwa mbele yangu, magurudumu niliyochagua hayakuwa mazuri.”
Ducati wanaongoza katika jedwali la kampuni huku nafasi ya pili na tatu ikishikiliwa na Yamaha na Aprilia mtawalia.
Matokeo ya mbio za pikipiki za Austrian MotoGP 2021
Mshindi: Brad Binder - KTM
Nafasi ya pili: Francesco Bagnaia - Ducati
Nafasi ya tatu: Jorge Martin - Ducati
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.