Macho yote kuangazia mbio za Belgian Grand Prix 2022


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship 

14 Round

2022 Belgian Grand Prix

Circuit de Spa-Francorchamps
Stavlot, Belgium 
Sunday, 28 August 2022
 
Mbio za langalanga za Belgian Grand Prix 2022 zinatarajiwa kufanyika Stavlot, ambao ni mji uliopo mkoa wa Liège, nchini Belgium Agosti 28.
 
Huu utakuwa mzunguko wa 14 wa msimu wa 2022 wa mashindano ya dunia ya Formula One na utafanyika katika mkondo wa Circuit de Spa-Francorchamps.
 
Mbio za Belgian Grand Prix ni mojawapo ya mbio maarufu kwenye ratiba ya Formula One kwa sababu ya mandhari ya kuvutia na ya kihostoria ya mkondo Spa-Francorchamps ambayo huvutia maderava na mashabiki.
 
Mbio za hivi karibuni katika ratiba ya msimu 2022 wa mashindano ya dunia ya Formula One zilikuwa Hungarian Grand Prix ambapo Max Verstappen aliibuka na ushindi mnamo Julai 31.

Carlo Sainz Jr
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Madereva wawili wa Mercedes, Lewis Hamilton na George Russell walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia huku timu ya Mercedes-AMG Petronas ikifurahia mbio nzuri Hungary.
 
Verstappen anashikilia nafasi ya kwanza katika jedwali la 2022 la madereva akiwa amezoa alama 258, huku akijaribu kutetea taji la dunia la Formula One.
 
Dereva wa Ferrari Charles Leclerc akiwa na alama 178 na dereva wa Red Bull Racing-RBPT Sergio Perez akiwa na alama 173 wanashikilia nafasi ya pili na tatu mtawalia zikiwa zimesalia mbio tisa za msimu huu.
 
Russell akiwa na158, Carlos Sainz Jr wa Ferrari akiwa na alama 156 na Hamilton akiwa na alama 146 wanashikilia nafasi ya nne, tano na sita mtawalia.

George RussellHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Naipongeza timu yangu sana ambao wamekuwa wakinisukuma na hawakukata tamaa mwaka huu ambao umekuwa na changamoto nyingi na kufanikiwa kuwa na magari mawili kwenye nafasi ya jukwaani mara mbili,” alisema Hamilton baada ya mbio za Hungarian Grand Prix.
 
"Imekuwa siku njema kwa upande wetu ila haikuwa nzuri sana kwa George. Madereva wengine wamekuwa na matokeo mazuri lakini tunajaribu kuwafikia. Inatia moyo kwenda kwenye mapumziko hasa baada ya matokeo kama haya.
 
"Ni matumaini yetu kuwa kipindi cha pili cha msimu tutaendelea na kasi hiyo hiyo ili kuweza kupambana na madereva wanaoshikilia nafasi za kwanza.”
 
Red Bull Racing-RBPT wanaongoza kwenye jedwali la waundaji magari huku wakifuatiwa na Ferrari na Mercedes mtawalia.
 

Matokeo ya mbio za Belgian Grand Prix 2021

 
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing-Honda 
Nfasi ya pili: George Russell - Williams-Mercedes 
Nafasi ya tatu: Lewis Hamilton - Mercedes 
 
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

 
 
 

Published: 08/25/2022