Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 1
Fulham v Liverpool
Craven Cottage
London, England
Saturday, 6 August 2022
Kick-off is at 1430
Liverpool watakuwa wageni wa Fulham ugani Craven Cottage wikendi ya ufunguzi wa msimu mpya wa
ligi ya premier 2022/23 huku wakipania kushinda taji dhidi ya Manchester City ifikapo mwisho wa msimu.
Mabingwa hao wa kombe la FA Cup walishinda kombe la kwanza la msimu walipoishinda Manchester City, mabingwa wa EPL 3-1 kwenye kombe la Community Shield wikendi iliyopita.
Jurgen Klopp anapania kuanza msimu kwa ushindi dhidi ya The Cottagers ambao walipanda daraja kwa kushindi ligi ya daraja la pili mara tu baada ya kushuka daraja.
Mara ya mwisho wakiwa kwenye ligi ya premier, Fulham hawakushindwa na Liverpool katika mechi zote mbili huku wakipata ushindi wa 1-0 uwanjani Anfield mnamo Machi 2021 baada ya sare ya 1-1 miezi kabla mjini London.
Sare ya Disemba 2020 ilifikisha kikomo msururu wa mechi sita bila kushinda dhidi ya Liverpool, na sasa Marco Silva atajaribu kupata ushindi Jumamosi hii ugani Craven Cottage.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Fulham ilimaliza mechi za kujiandaa kwa msimu mpya kwa kupata sare ya 1-1 dhidi ya Villarreal, Marco Silva akikiri kufurahishwa na mchezo wa timu yake kuelekea mchezo dhidi ya The Reds.
"Tulimaliza maandalizi yetu dhidi ya timu inayoshiriki mechi za ligi ya klabu bingwa ulaya na tulifahamu uwezo walio nao,” raia huyo wa Ureno alisema. “Tulipata nafasi nzuri lakini hatukuzitumia vilivyo lakini tuna nafasi ya kujiimarisha.
"Hatukutakiwa kuwa 1-0 chini kipindi cha kwanza. Tulikosa kasi tuliyokuwa nayo katika kipindi cha pili lakini tulipambana zaidi na kubadilisha matokeo. Ulikuwa mchezo mzuri dhidi ya timu nzuri na tumejifunza mengi.”

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Klopp anakiri kuwa bado wana kazi ya kufanya wiki zijazo ili kujiweka tayari ratiba itakayojumuisha kucheza mechi tatu kwa wiki.
"Nafahamu kuna kazi kubwa ya kufanya. Kama tulivyosema awali, tunafaa kuongeza muda wa maandalizi kwa ajili ya msimu mpya kwa wiki mbili zaidi ila hatukufaulu,” alisema raia huyo wa Ujerumani.”
"Hatuwezi kuwa na mtiririko wetu wa kawaida pasipo na maandalizi mazuri. Hatuwezi kucheza mechi za wikendi iwapo hatujajiandaa vizuri. Baada ya wiki tatu au nne tutaanza kucheza mechi tatu kwa wiki.”
Takwimu baina ya timu hizi kwenye mechi tano za ligi zilizopita
Mechi - 5
Fulham - 1
Liverpool - 3
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.