Debi ya London kufanyika Jumapili hii


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 2

Chelsea v Tottenham Hotspur

Stamford Bridge
London, England
Sunday, 14 August 2022
Kick-off is at 18h30 
 
Tottenham watakuwa mgeni wa Chelsea ugani Stamford Bridge Jumapili ya Agosti 14 katika mechi ya ligi kuu Uingereza.  
 
The Blues walianza msimu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park ambapo penalti kutoka kwa kiungo Jorginho kunako dakika ya 45 kuliipa ushindi Chelsea dhidi ya meneja na mchezaji wao wa zamani, Frank Lampard.
 
Vijana wa Thomas Tuchel walikuwa na matokeo mseto kwenye mechi za kujiandaa kwa msimu mpya; ushindi dhidi Club America pamoja na Udinese lakini pia walipoteza dhidi ya Arsenal na Charlotte, huku Tuchel akikiri kuwa bado wana nafasi ya kuimarika zaidi japokuwa alifurahishwa na uchezaji wa timu yake dhidi ya the Toffees.

Thomas Tuchel
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Ushindi wa aina yoyote ni mzuri na unawezesha kupanua upeo wa mawazo na nafasi ya kuimarika zaidi. Kuna vitu vingi vya kujifunza,” alisema Tuchel.
 
"Kuna mafunzo muhimu ya kujifundisha. Huu umekuwa uwanja mgumu kwa Chelsea kupata alama zote misimu michache iliyopita na tumefanikiwa kupata alama zote bila kuruhusu goli.”
 

Kileleni mwa msimamo na nafasi ya kushinda zawadi bab-kubwa

Chomoka na Odds msimu huu na unaweza kushinda mgao wa mamilioni ya zawadi.
Kuanzia pesa taslimu hadi Free Bets na mzigo wa vifaa vya nyumbani ikiwemo TV, home theatre, jiko na mashine ya kufulia, kuna mechi nyingi za kubashiri kila wiki.

Chomoka na Odds
 
Kwengineko, Spurs wamekuwa na matokeo mabaya dhidi ya Chelsea kwenye mechi za hivi majuzi baada ya kucheza mechi saba bila ushindi tangu Novemba 2018.
 
Timu hiyo ya Antonio Conte ikiwa nyumbani ilitoka nyuma na kupata ushindi wa 4-1 dhidi ya Southampton katika mechi yao ya kwanza ya msimu.

Antonio Conte
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Conte alifurahishwa na jinsi vijana wake walivyojituma baada ya kufungwa dakika ya 12 na James Ward-Prowse na jinsi timu yake ilivyoimarika katika kipindi cha miezi saba tangu aliposhika usukani.
 
"Tulianza mchezo vizuri licha ya kufungwa goli mapema. Soka haitabiriki. Hatukustahili kufungwa kwa sababu tulianza mchezo vizuri,” raia huyo wa Italia aliambia SPURSPLAY.
 
"Ulikuwa wakati mwafaka wa kuona wachezaji wetu watakavyojizoa baada ya kufungwa. Tulionyesha ukakamavu, utulivu na kutengeneza nafasi za kufunga mabao na tulifanikiwa kufunga mabao mawili.
 
"Leo nimeshuhudia matukio ya kufurahisha. Tumekuwa tukijifundisha mbinu na mambo mengine ili kujiimarisha zaidi; kasi ya mchezo na kuzuia tunapopoteza mpira.”
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili, mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Chelsea - 4
Tottenham - 0
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 08/11/2022