City watafuta ushindi wa kwanza dhidi ya Reds tangu 1993


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 5

Manchester City v Nottingham Forest

Etihad Stadium
Manchester, England
Wednesday, 31 August 2022
Kick-off is at 21h30  
 
Manchester City watazamia kuendeleza ubabe wao kwenye ligi watakapowaalika Nottingham Forest ugani Etihad Stadium Jumanne Agosti 31.
 
Vijana wa Pep Guardiola tayari wamepoteza alama mbili msimu huu baada ya kupata sare ya 3-3 dhidi ya Newcastle St James' Park katika mechi ya pili ya msimu.
 
Kwa mechi ya pili mfululizo msimu huu, The Citizens walijikuta nyuma Jumamosi John Stones alipojifunga goli dakika ya nne dhidi ya Crystal Palace kabla ya Joachim Andersen kuongeza goli la pili kwa faida ya wageni.
 
Hata hivyo Bernardo Silva alifungia City goli la kwanza dakika ya 53 huku Erling Haaland akifunga magoli matatu; 62', 70', 81, ushindi unaowaweka kwenye nafasi ya pili, alama mbili nyuma ya viongozi Arsenal.  

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Guardiola alisifia mchango wa sajili mpya Haaland, ambaye kwa sasa amefanikiwa kufunga magoli matano katika ligi, huku magoli yake ya kwanza mawili yakija dhidi ya West Ham United.
 
"Erling amekuwa akifunga magoli tangu zamani,” alisema raia huyo wa Uhispania. “Amekuwa akifanya hivyo Salzburg na kila sehemu aliyokuwa.
 
"Mara nyingi tunakuwa na wakati mgumu dhidi ya timu kama hizi kwa sababu wanazuia sana ila ana uwezo wa kufungua nafasi hizo. Magoli yote matatu, hasa la kwanza yalikuwa mazuri.
 
"Amekuwa akifunga magoli mengi sana. La muhimu ni kuwa ameingiliana vizuri na ligi na ni mchezaji mnyenyekevu.”
 

Kileleni mwa msimamo na nafasi ya kushinda zawadi bab-kubwa

Chomoka na Odds msimu huu na unaweza kushinda mgao wa mamilioni ya zawadi.
Kuanzia pesa taslimu hadi Free Bets na mzigo wa vifaa vya nyumbani ikiwemo TV, home theatre, jiko na mashine ya kufulia, kuna mechi nyingi za kubashiri kila wiki.

Chomoka na Odds
 
Forest wamefanikiwa kupata ushindi mmoja tu kwenye mechi nne za kwanza za ligi tangu walipopandihswa ila wanaonyesha uchezaji mzuri.
 
Timu hii ya Steve Cooper iliwapa wakati mgumu Tottenham wakati wa mechi ya Jumapili ambapo Harry Kane alifunga magoli mawili kwenye mechi iliyoishia 2-0.

Steve Cooper
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Cooper amekiri kuwa timu yake iliruhusu magoli mawili ya rahisi japokuwa aliona mambo mengi ya kufurahisha kutokana na uchezaji wa timu yake.
 
"Kulikuwa na mambo mengi ya kujivunia ambayo tulifanya vizuri leo,” alisema. “Hatukupata matokeo tuliyokuwa tunatarajia kwenye mechi japo tulicheza vizuri. Cha muhimu ni ushindi.
 
"Kwa bahati mbaya tuliruhusu goli moja la mapema. Tuliendelea na kucheza kama tulivyokuwa tumepanga na kuwadhibiti. Harry Kane alijipata kwenye eneo zuri na kutuadhibu.
 
"Goli la pili lilitokana na uzembe wetu wa kuzuia vizuri. Tuliruhusu mipira kuja kwenye kisanduku kwa urahisi. Licha ya mapungufu hayo, kulikuwa na mengi ya kujifunza kutokana na mechi hiyo.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Man City - 1
Notts Forest - 2
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 08/31/2022