Blues wapania kuongeza masaibu zaidi kwa Foxes


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 4

Chelsea v Leicester City

Stamford Bridge
London, England
Saturday, 27 August 2022
Kick-off is at 17h00 
 
Chelsea wananuia kupata ushindi kwenye mechi ya ligi dhidi ya Leicester watakapokabiliana ugani Stamford Bridge Jumamosi Agosti 27.
 
The Blues walipata kichapo cha 3-0 mikononi mwa Leeds ugani Elland Road Jumapili iliyopita ambapo pia mchezaji mpya Kalidou Koulibaly alionyeshwa kadi nyekundu huku zikisalia dakika sita mchezo kukamilika.
 
Vijana wa Thomas Tuchel walianza msimu mpya kwa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Everton kabla ya kupata sare ya 2-2 dhidi ya Tottenham. Hii ni baada ya Harry Kane kufunga goli la kusawazisha dakika za lala salama.
 
Kwa sasa, Chelsea wana alama nne wakiwa kwenye nafasi ya kumi na mbili katika jedwali la ligi. Ni alama tano nyuma za viongozi Arsenal ambayo ni timu ya pekee hadi sasa iliyoweza kupata ushindi wa mechi tatu za kufungua msimu.

Thomas TuchelHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Tuchel alisema kushindwa kwao kulitokana na kukosa nidhamu ya mchezo katika dakika za kwanza 20 ambapo waliwapa wapinzani wao nafasi ya kutawala kipindi hicho.
 
"Mtiririko wetu ulipotea dakiaka za kwanza 20. Tulikuwa na nafasi nyingi za kufunga goli moja au mawili lakini tulipoteza nidhamu ya mchezo. Tuliacha kutilia mkazo mbinu na mpango tuliokuwa nao wa kuwadhibiti wapinzani wetu,” alisema raia huyo wa Ujerumani.
 
"Mechi iligeuka na sasa tulikuwa tunacheza katika kiwango kimoja badala kuwa magoli mawili mbele. Tuliruhusu magoli mawili ya rahisi sana. Kwa hali hii, imani na hari ya mpinzani inakuwa juu na mechi inakuwa ngumu.”
 
The Foxes wamekuwa na matokeo mabovu tangu kuanza kwa msimu huu kwani wamepata alama moja tu katika mechi tatu za kwanza za msimu huu.
 
Timu ya Brendan Rodgers ilipoteza mechi dhidi ya Southampton 2-1 uwanjani King Power Stadium baada ya kutangulia kufunga. Hii ilikuwa mechi ya pili kwao kupoteza msimu huu na mechi ya tatu ya ligi bila ushindi.

Brendan Rodgers - Leicester manager
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mashabiki wa klabu hiyo walionyesha kutoridhika kwao na uchezaji wa timu yao baada ya mpira kuisha kwani walionekana kuwarushia cheche za maneno. Kocha Brendan Rodgers alisema anaelewa kutoridhika kwa mashabiki ukizingatia kuna wachezaji kadhaa wa timu ya kwanza ambao bado wanajaribu kuweka sawa kantarasi zao.
 
"Ni wakati mgumu kwetu sasa hivi. Hilo halina shaka,” Rodgers aliambia Sky Sports.
 
"Klabu hii imekuwa na matokeo mazuri miaka michache iliyopita ikipambana na timu kubwa na kushinda mataji. Mashabiki walikuwa na matumaini makubwa na walitarajia timu itasajili wachezaji wapya ili kuendelea kukua na kupata mafanikio zaidi.

Kileleni mwa msimamo na nafasi ya kushinda zawadi bab-kubwa

Chomoka na Odds msimu huu na unaweza kushinda mgao wa mamilioni ya zawadi.
Kuanzia pesa taslimu hadi Free Bets na mzigo wa vifaa vya nyumbani ikiwemo TV, home theatre, jiko na mashine ya kufulia, kuna mechi nyingi za kubashiri kila wiki.

Chomoka na Odds
 
"Hatujafanikiwa kufanya hivyo. Ni kipindi kigumu hivyo basi naelewa mashabiki wanapoonyesha kutoridhika kwao kwani wanataka kuona timu yao ikikua siku hadi siku.”
 
"Wachezaji wenyewe wangependa kuwa na ushindani baina yao katika nafasi mbalimbali kwenye timu. Kwa sasa tutazingatia kufanya kazi na wachezaji tulionao hapa na wameonyesha kuwa wako tayari kusaidia timu kurekebisha matokeo.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Chelsea - 2
Leicester - 1
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 
 
 

Published: 08/25/2022