Barca na Sociedad kukabana koo


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Spanish La Liga

Matchday 2

Real Sociedad v Barcelona

Reale Arena
San Sebastian, Spain
Sunday, 21 August 2022
Kick-off is at 23h00 
 
Barcelona watakuwa wageni wa Real Sociedad ugani Reale Arena kwenye mechi ya ligi mnamo Agosti 21, Jumapili.
 
Katika mechi ya kwanza ya msimu, vijana wa Xavi walitoka sare ya 0-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Rayo Vallecano Jumamosi iliyopita.
 
Mahasimu wao Real Madrid walikuwa miongoni mwa timu tano zilizopta ushindi kwenye mechi za kufungua msimu. Barcelona watanuia kupungaza nafasi hiyo katika mechi ya pili ya msimu.

XaviHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Xavi alikiri kuwa timu yake haikucheza katika viwango vinavyostahili na kuwasihi mashabiki kuwa wavumilivu. Hata hivyo, alihisi Vallecano walistahili pongezi kwa kuwadhibiti.
 
"Hutukucheza vizuri. Tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzitumia vilivyo. Tumepata alama moja tu na haitoshi. Sharti tuendelee kujituma na kuamini mbinu zetu,” Xavi alisema
 
"Safu ya ulinzi ya Rayo ilikuwa dhabiti na mlindalango wao alikuwa na mchezo mzuri kabisa. Hatukuwa na mchezo mzuri japo kila mchezaji alijaribu sana.  
 

Kileleni mwa msimamo na nafasi ya kushinda zawadi bab-kubwa

Chomoka na Odds msimu huu na unaweza kushinda mgao wa mamilioni ya zawadi.
Kuanzia pesa taslimu hadi Free Bets na mzigo wa vifaa vya nyumbani ikiwemo TV, home theatre, jiko na mashine ya kufulia, kuna mechi nyingi za kubashiri kila wiki.

Chomoka na Odds
 
"Tuliadhirika na unyevunyevu na joto sawa na Rayo. Tunawauliza mashabiki wa timu hii kuwa watulivu.”
 
Real Sociedad walianza msimu vizuri kwa kuwashinda Cadiz 1-0 ugani Nuevo Mirandilla Jumapili. Goli lilifungwa na Takefusa Kubo dakika ya 24.
 
Hata hivyo, rekodi yao dhidi ya Barcelona ni mbovu kwani wamepoteza mechi tano za mwisho dhidi ya mpinzani huyo.

Imanol Alguacil
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kocha wa Sociedad Imanol Alguacil alikuwa na furaha kwa kupata alama tatu za kwanza japokuwa alihisi wangeshinda kwa magoli mengi.
 
"Tumeanza msimu vizuri dhidi ya timu ngumu. Tulitaka kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kila tulipopata fursa,” alisema Alguacil.
 
"Nina furaha japo kidogo kwa sababu matokeo yalikuwa mazuri. Kipindi cha kwanza hatukujituma vilivyo katika kutafuta goli kwa sababu haikuwa rahisi. Timu hii ina wachezaji wazuri walio na uwezo wa kufunga magoli zaidi.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano zilizopita za ligi

Mechi - 5
Sociedad - 0
Barcelona - 5
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 
 
 

Published: 08/17/2022