Zote za kukimbia kwa mens 4x100m


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Michezo ya Olimpiki 2020

Julai 23- Agosti 8, 2021

Tokyo, Japan 
 
Mbio za wanaume za 4x100m kupokezana vijiti zinatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye michezo wa Olimpiki mjini Tokyo, lakini imekuwa vigumu kubashiri  nani wataibuka mabingwa.  
  
Kabla ya michezo kuanza Marekani walionekana dhahiri wangekuwa washindi wa dhahabu katika mbio hizo, lakini kutetereka kwa mkali wao Trayvon Bromell kwenye mbio za mita 100 kumewapa wapinzani wa Marekani matumaini.
  
Mwanariadha wa Afrika Kusini Akani Simbine
 Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 
Hata hivyo, Marekani bado inatarajiwa kuwa na nguvu zaidi. Bromell bado anashikilia rekodi ya muda wa kasi zaidi mwaka huu licha ya kushindwa kufuzu fainali ya mbio za mita 100 nchini Japan. Wenzake wawili- Fred Kerley aliyeshinda fedha na Ronnie Baker aliyemaliza kwenye nafasi ya tano walifuzu fainali, na wameonyesha wako katika hali nzuri.
  
Pia wanaweza kumtegemea mtaalamu wa mbio za mita 200 Noah Lyles, ambaye alikua katika timu ya Marekani iliyoshinda  ubingwa wa dunia 2019 mjini Doha.
 
Zharnel Hughes ni mwingine anayetazamia kurekebisha makosa aliyofanya katika mita 100. Mwanariadha huyo Muingereza aliondolewa kwenye fainali hiyo kwa kosa la kuanza visivyo, lakini atapenda kutumia mbio za kupokezana vijiti kulipiza kisasi. Alikuwa katika kikosi kilichoweka muda bora zaidi mwaka huu katika mashindano yaliyofanyika Gateshead, Uingereza mwezi uliopita.
 
Afrika Kusini ndio mabingwa wa mbio hizo za kupokezana vijiti kwa sasa kufuatia ushindi wao nchini Poland mwezi Mei lakini watamkosa Gift Leotlela aliyepata jeraha kwenye nusiu fainali za mita 100.
  
Matokeo yake ni kwamba Afrika Kusini itamtegemea sana Akani Simbine, aliyemaliza wa nne kwenye fainali.
  
“Aliye bora zaidi ndiye aliyeshinda. Nimeudhika. Lakini nilifika fainali. Kosa la kuanza visivyo halikuniathiri mimi. Inabidi kujipanga upya na kuendelea” alisema Simbine siku ya Jumapili, huku akionekana kuudhika.

Jamaica ndio wanaonekana dhahiri wenye uwezo wa kushinda mbio za wanawake za 4x100m, baada ya kushinda dhahabu, fedha na shaba mwishoni mwa wiki.
 
Mchujo wa mbio hizo kwa wanawake na pia wanaume utaanza Alhamisi, huku fainali ikitarajiwa kufanyika Ijumaa mjini Tokyo.


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 08/05/2021