Hakimiliki ya picha: Getty Images
Udinese v Juventus
2021-22 Serie A
Siku ya 1
22 Agosti 2021
Dacia Arena, Udine
19:30
Timu za Udinese na Juventus zitafungua msimu wa ligi kuu ya
Italia- Serie A zitakapokutana katika mtanange uitwao derby ya ‘michirizi nyeusi na nyeupe’ kwenye uwanja wa Dacia Arena mjini Udine Jumapili Agosti 22 jioni, kuanzia saa 19:30. Ni mojawapo ya mechi zitakazochezwa wikendi ya tarehe 21-23 Agosti kufungua msimu wa Serie A wa 2021-22.
Udinese haikufanya vizuri msimu uliopita wa 2020-21; walimaliza kwenye nafasi ya 14 wakiwa na alama 40. Matumaini ya kuimarika katika msimu mpya yamepata pigo baada ya wachezaji wao wa kutegemewa Rodrigo de Paul na Juan Musso kuondoka.
Hata hivyo, meneja Luca Gotti anaamini timu yake inaweza kushindana vizuri na timu zilizoko kwenye nusu ya pili ya orodha ya msimamo wa ligi ya Serie A: “Tumesema mara nyingi tuna utashi wa kubadilika. Lakini kwa sababu mazingira yanayohitaji kutangulia mabadiliko hayo hayapo, kwa sasa tunaendelea kama tulivyo.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Miamba Juventus pia walikuwa na msimu mbaya wa 2020-21, wakamaliza kwenye nafasi ya nne na wakakosa ubingwa wa ligi ambao ungekuwa wa mara ya 10 mtawalia. Sasa wamemrejesha Max Allegi kama meneja, na ingawa hawajatumia hela nyingi kusajili, wanaanza msimu wakionekana timu bora yenye uwezo wa kushinda ligi.
Hata hivyo, mlinzi wao wa miaka mingi Leonardo Bonucci anasisitiza ushindani uko wazi na timu kadhaa zina uwezo wa kuibuka mabingwa: “
Intermilan wanaweza kwa sababu walishinda, hata bila kuwa na Romelu Lukaku na Achraf Hakimi. Lakini Lazio wakiwa na meneja Maurizio Sarri, watataka kuwakomesha Roma ya Mourinho. Milan wenyewe wamenunua wachezaji kuonyesha uongozi wao. Utakuwa msimu wa kusisimua.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Takwimu zinaonyesha Udinese na Juventus zimekutana mara 53 katika mashindano yote tangu 1997. Juventus wameshinda mara 37 ikilinganishwa na tisa za Udinese, na mechi saba zimeishia sare.
Msimu uliopita Juve waliwafunga Udinese nyumbani na ugenini, wakashinda 4-1 mjini Turin Januari 2021, kisha wakawafunga 2-1 mjini Udine Mei 2021, huku Christiano Ronaldo akifunga jumla ya goli nne katika mechi hizo mbili.
Udinese v Juventus – Takwimu
Mechi zilizochezwa: 53
Udinese wakashinda: 9
Juventus wakashinda: 37
Sare:7
Odds bomba za kubashiri mpira wa miguu na machaguo yaliyoboreshwa zaidi, kubashiri michezo haijawahi kuwa rahisi hivi, Jisajili uanze kushinda na Betway! Jiunge na Betway sasa ubashiri La Liga kwa Free Bet TSh 3,000.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway