Pacquiao atafuta ushindi wa nne mtawalia


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Manny Pacquiao v Yordenis Ugas

Ubingwa wa WBA (Super) Welterweight 

T-Mobile Arena, Las Vegas, United States
22 Agosti 2021
Pigano linaanza 04:00 
 
Bondia Manny Pacquiao atakuwa anafuata ushindi wa mara ya nne mtawalia atakapopigana na Yordenis Ugas pigano la ubingwa wa dunia wa WBA (Super) Welterweight katika ukumbi wa T-Mobile mjini Las Vegas, Marekani, Jumapili tarehe 22 Agosti 2021. 
  
Pacquiao ni bondia pekee katika historia aliyewahi kutwaa ubingwa wa dunia mara nane katika uzani tofauti, na hajapigana tangu alipotangazwa mshindi dhidi ya Keith Thurman Julai 2019 bila kupigana. Pigano hilo lilipangiwa kuwa dhidi ya bingwa wa dunia wa IBF na WBC Welterweight Errol Spence Jr, lakini bondia huyo akalazimika kujiondoa kutokana na jeraha la jicho.
  
Spence alisema alitazamia pigano hilo lakini “haingewezekana kupigana jicho langu likiwa katika hali ile.”
  
Bondia wa Cuba Yordenis Ugas
 Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
"Kwanza kabisa, namuomba kila mtu aungane nami katika kumuombea Errol Spencer Jr apone kabisa,” Pacquiao alisema. 
 
"Shukuru Mungu kwamba hali ya jicho lake iligunduliwa kwa kuangaliwa, kabla ya kuharibika zaidi. Nimekubali kupigana na Yordenis Ugas Agosti 21 (22 eneo la CAT) kuwania ubingwa wa dunia wa WBA Welterweight Super. Njia sahihi na njia pekee ya kushinda taji la dunia ni kupigana ulingoni.”
 
‘Pacman’ mwenye umri wa miaka 42 alitwaa taji la dunia la WBA alipomshinda Thurman miaka miwili iliyopita, lakini akapokonywa mwezi Januari kwa sababu ya kukaa muda mrefu bila kupigana. 
  
Hii ilimwezesha Ugas kutawazwa bingwa wa taji hilo baada ya taji alililokuwa nalo la Regular alilotwaa kwa kumshinda Abel Ramos mwaka uliopita kupandishwa hadhi Pacquiao alilipokonywa taji lake.
  
Bondia wa Marekani Errol Spence Jr
 Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
Ugas mwenye umri wa miaka 35, na ambaye anatokea Santiago de Cuba, alishinda medali ya shaba kwenye michezo ya Olimpiki ya 2008 mjini Beijing na alitawazwa bingwa wa dunia wa Amateur Lightweight mwaka wa 2005. 
  
Pia naye anafukuzia taji la nne mtawalia na anapania kujiunga na mabondia Jeff Horn, Floyd Mayweather Jr, Juan Manuel Marquez, Timothy Bradley, Erik Morales, Medgoen Singsurat na Rustico Torrecampo ambao wamewahi kumshinda Pacquiao.
 
"Kwa wale mlionikejeli Pacquiao aliporejea na kutangaza kupigana na Spence. Nataka kuwapa zawadi ya pigano la kupendeza,” alisema Ugas.
 

Ulinganifu wa mabondia hawa

  

Manny Pacquiao

 
Jina la utani: PacMan
Nchi: Filipino
Umri: 42
Rekodi: 62-7-2 (39 KO)
Urefu:168 cm
Reach: 170cm
Stance: Southpaw
  
- Bondia pekee katika historia bingwa wa dunia uzani nane tofauti
  
- Mshindi wa mataji 12 ya dunia
  

Yordenis Ugas

 
Jina la utani: 54 Milagros
Nchi: Cuba
Umri: 35
Rekodi: 26-4 (12 KO)
Urefu: 175cm
Reach: 175cm
Stance: Orthodox
 
- Bingwa wa sasa wa WBA (Super) Welterweight 
 
- Bingwa wa zamani wa dunia uzani wa lightweight amateur 
 

 Bashiri ndondi na Betway


Tunakuletea mapambano bora ya ndondi na unaweza kubashiri kwa kutumia simu au kompyuta yako. Weka ubashiri wako kwa urahisi na uwashangilie mabondia unaowapenda kiganjani mwako. Betway inakupa kile unachotaka kwenye Ulimwengu wa kubashiri ndondi live. Rusha ngumi na ingia ulingoni nasi tunakupa odds nono. Bashiri kwenye mapambano makubwa na Betway Tanzania.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

 

 

Published: 08/19/2021