Hakimiliki ya picha: Getty Images
Msimu wa 2021, Ubingwa wa Dunia MotoGP
Uholanzi MotoGP
Awamu ya 11
Red Bull Ring
Spielberg, Austria
Jumapili, Agosti 15, 2021
Mashindano ya mbio za pikipiki ya
Austrian MotoGP ambayo pia yanajulikana kama Bitci Motorrad Grand Prix von Österreich yatafanyika katika mji wa Spielberg, Austria Agosti 15.
Itakuwa awamu ya 11 ya mfululizo wa mashindano ya mwaka huu na yamepangiwa kufanyika katika uwanja wa Red Bull Ring.
Mashindano ya hivi karibuni msimu huu Styrian Grand Prix pia yalifanyika katika uwanja huo wa Red Bull Ring kutokana na kufutwa kwa mashindano ya Finnish Grand Prix.
Katika mashindano ya mwaka uliopita ya Austrian MotoGP mshindi alikuwa Andrea Dovizioso wa timu ya Ducati akifuatiwa na Joan Mir wa Suzuki, naye mwendashi wa Ducati Jack Miller akawa wa tatu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Na kwenye mashindano ya karibuni ya Styrian MotoGP yaliyofanyika Agosti 8, na ambayo yalikuwa ya kusisimua mshindi alikuwa Jorge Martin wa timu ya Ducati.
Martin, ambaye huo ulikuwa ushindi wake wa mara ya kwanza alifuatiwa na Mir kwenye nafasi ya pili naye mwendeshaji wa Yamaha Fabian Quartararo akamaliza katika nafasi ya tatu.
Quartararo yuko kileleni kwenye msimamo wa waendeshaji msimu huu wa 2021 akiwa amekusanya alama 172 huku mpambano wa taji la dunia ukiendelea.
Mwendeshaji wa Ducati Johann Zarco (alama 132) anashikilia nafasi ya pili naye bingwa mtetezi Mir (alama 121) yuko katika nafasi ya tatu kwenye msimamo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Martin, ambaye kwa sasa ni wa 12 kwenye msimamo, alionyesha furaha kubwa baada ya kushinda mashindano ya Austrian Grand Prix akiwa anashiriki mashindano ya daraja hilo kwa mara ya kwanza.
“Imekuwa wikendi nzuri sana kwangu. Kufanikiwa kuanza kwenye nafasi ya Pole, na sasa ushindi ni jambo la ajabu kweli. " Martin alisema.
"Ni furaha isiyoelezeka kuwa mshindi katika MotoGP nikishiriki mara ya kwanza, nimefanikiwa. Ushindi wa mara ya kwanza na kupanda jukwaani mara moja ni mafanikio makubwa, na natumai tutaendelea hivyo.”
"Kwenye mizunguko ya mwisho nilikuwa nafikiria vitu vingi. Ndio sababu sikufanya vizuri mizunguko ya mwisho, lakini kulikuwa na mwanya wa kukabiliana nao."
Katika msimamo wa timu, Yamaha wanaongoza wakifuatiwa na Ducati, nao KTM ni wa tatu.
Matokro ya Austrian MotoGP 2020
Mshindi: Andrea Dovizioso - Ducati
Mshindi wa pili: Joan Mir - Suzuki
Nafasi ya tatu: Jack Miller - Ducati
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni
soka,
motorsport,
mpira wa kikapu,
rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway