Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021 US Open
ATP Tour & WTA Tour
USTA Billie Jean King National Tennis Center
New York City, USA
30 Agosti - 12 Septemba 2021
Mashindano ya
Tennis ya US Open 2021 yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa kitaifa wa Tennis wa USTA Billie Jean King kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 12.
Yatakuwa Makala ya 141 ya mashindano ya US Open na pia ni mashindano makubwa yaani Grand Slam ya nne na ya mwisho kufanyika mwaka huu.
Pia yatakuwa mashindano ya kwanza ya Grand Slam tangu yale ya Australian Open 1997 kufanyika bila Roger Federer, Rafael Nadal, Serena Williams, au Venus Williams katika droo kubwa ya mchezaji mmoja mmoja.
Mashindano hayo hufanyika kwenye sakafu ngumu na huandaliwa katika viwanja 15 ambavyo vina sakafu ya DecoTurf.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Dominic Thiem ndiye bingwa mtetezi upande wa wanaume naye Naomi Osaka anatetea taji upande wa kina dada baada ya wote wawili kutwaa ubingwa mwaka uliopita.
Hata hivyo, Thiem, ambaye ni mmoja wa wanatennis Hodari kabisa duniani kwa wakati huu, amejiondoa kutoka mashindano ya mwaka huu kutokana na jeraha la mkono.
Wachezaji magwiji kama Novak Djokovic, Daniil Medvedev, Stefanos Tsitsipas, Dominic Thiem, Alexander Zverev na Andrey Rublev wanatafuta taji hilo la Thiem.
Ingawa Osaka anapania kutetea taji la wanawake, lakini wapo kina dada wanaolitaka taji hilo sana kama vile Ashleigh Barty, Aryna Sabalenka, Elina Svitolina, Bianca Andreescu, na Iga Świątek na tayari wako New York.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Naomi Osaka aliamua kukataa kujitokeza mbele ya waandishi wa habari kwenye mashindano ya French Open kwa sababu ya wasi wasi kuhusu afya ya kiakili na kukawa na mjadala kuhusu jinsi mikutano na waandishi kwenye mashindano makubwa ya Grand Slams itakavyokuwa inaendeshwa.
Hata hivyo, mkurugenzi mkuu wa US open Stacey Allaster ameweka wazi kwamba itakuwa lazima kuhudhuria mikutano na waandishi wa habari.
"Wachezaji kujitokeza mbele ya waandishi wa habari ni jambo muhimu kwa mashabiki wetu," Allaster alisma.
"Hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya itifaki, mambo yataendeshwa sawa kwa kila mchezaji. Lakini mabadiliko yatakuwepo katika swala la afya ya wachezaji. Hilo tumefanya siku zilizopita.
"Mchezaji anapopata jeraha au akiwa hawezi kuhudhuria kikao na waandishi, tathmini ya kitabibu itafanyika na madaktari kutoa uamuzi."
2020 US Open fainali ya wanaume
Dominic Thiem alimshinda Alexander Zverev
2020 US Open fainali ya wanawake
Naomi Osaka alimshinda Victoria Azarenka
Bashiri tenisi mtandaoni
Bashiri manguli kwenye michuano bora ya tenisi kutoka Wimbledon hadi Roland Garros. Jisajili leo na anza kubashiri kwenye machaguo tofauti ambayo tenisi inakupatia; kutoka 1x2 matokeo ya mechi, bashiri kwa mchezaji wako unayempenda hadi kwenye bashiri nyingi kama Mshindi wa Set. Chochote unachochagua kufanya, Betway ina chaguo kwaajili yako.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway