Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Ligi kuu ya England
Wiki ya 3
Manchester City vs Arsenal
Etihad Stadium
Manchester, England
Jumamosi, Agosti 28 2021
Itaanza 14:30
Manchester City wanalenga kuwaongezea Arsenal dhiki ya mwanzo mbaya wa msimu timu hizo mbili zitakapokutana kwenye mechi ya
ligi kuu ya England katika uwanja wa Etihad Jumamosi hii.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
City, baada ya kuanza ligi kwa kupoteza dhidi ya Tottenham walirejea kwa nguvu mechi iliyofuata na kuwazaba Norwich 5-0 na sasa mabingwa hao watetezi wanawakaribisha Arsenal timu inayolemewa kwa sasa.
Arsenal hawana alama hata moja baada ya kupoteza 2-0 mechi mbili mfululizo dhidi ya Brentford na Chelsea. Meneja Mikel Arteta tayari anakabiliwa na shinikizo na mambo hayatakuwa rahisi karibuni.
"Walikuwa timu bora. Ni mojawapo ya nyakati ngumu. Hali ni ngumu kiasi hatujapata kuona,'' Alisema Arteta baada ya kufungwa na Chelsea.
"Kujihurumia hakusaidii chochote. Inabidi ushinde mechi, utulie na kuonyesha moyo wa kujituma,''
Hakimiliki ya picha: Getty Images
City wameshinda mechi nyingi zaidi dhidi ya Arsenal katika misimu kadhaa iliyopita ya ligi kuu ya England na msimu uliopita wa 2020/21 walishinda mechi zote mbili nyumbani na ugenini. Raheem Sterling amefunga katika mechi nne mtawalia dhidi ya Arsenal na akafunga goli pekee katika mechi mbili kati ya timu hizo msimu uliopita.
Takwimu za Manchester City vs Arsenal:
Idadi ya Mechi:183
Manchester City wakashinda: 52
Arsenal wakashinda: 89
Sare: 42
Ratiba ya Mechi za Ligi kuu ya England, wiki ya 3
Jumamosi, 28 Agosti 2021
14:30 - Manchester City vs Arsenal
17:00 - Newcastle United vs Southampton
17:00 - Brighton & Hove Albion vs Everton
17:00 - West Ham United vs Crystal Palace
17:00 - Norwich City vs Leicester City
17:00 - Aston Villa vs Brentford
19:30 - Liverpool vs Chelsea
Jumapili, 29 Agosti 2021
16:00 - Burnley vs Leeds United
16:00 - Tottenham Hotspur vs Watford
18:30 - Wolverhampton Wanderers vs Manchester United
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway