Fabio Quartararo apania kuendlea kuongoza


Image copyright: Getty Images
 

Mashindano ya Dunia ya Mbio za Pikipiki- MotoGP 2021

Mkondo wa 10, Styrian Grand Prix

Jumapili, Agosti 2021
Red Bull Ring, Spielberg, Austria
 
Mwendeshaji Pikipiki wa timu ya Monster Energy Yamaha Fabio Quartararo anatazamia kuendelea kuongoza Mashindano ya Dunia ya mbio za pikipiki – MotoGP 2021 kwenye mkondo wa 10 wa Styrian Grand Prix, katika eneo maalum la Red Bull Ring mjini Spielberg, Austria alasiri ya Jumapili tarehe 8 Agosti, 2021.
  
Quartararo amekuwa akihodhi mshindano ya MotoGP mwaka huu, baada ya kushinda mara nne mashindano tisa yaliyofanyika, na pia mara nne akamaliza miongoni mwa sita bora. Mfaransa huyo anaongoza msimamo akiwa na alama 156, akiamuacha kwa alama 34 mpinzani wa karibu, Mfaransa mwenzake Johann Zarco wa timu ya Pramac Ducati.
  
Mwendeshaji wa Paramc Ducati, Johann Zarco
 Image copyright: Getty Images
  
Quartararo mwenye umri wa miaka 22 anatumai kuwa timu yake ya Yamaha itatoa matokeo bora katika mzunguko wa Red Bull Ring kama ilivyokuwa kwenye mashindano yaliyopita nchini Uholanzi, ambapo walishinda ubingwa wa Dutch TT mjini Assen, mwezi June. 
  
“Kusema kweli, barabara za mzunguko wa Austria ulikuwa mbaya kwetu mwaka uliopita, lakini nadhani zaidi ilitokana na matatizo tuliyokuwa nayo katika kupiga breki,’ alisema  Quartararo. “Kwangu mimi, pikipiki yangu imeimarika sana katika kupiga breki. Kifaa chetu cha holeshot cha kuongezea kasi pia kinafanya kazi vizuri. Vifaa vyote vya Elektroniki pia.
  
Mwendeshaji wa Lenovo Ducati, Francesco Bagnaia
 Image copyright: Getty Images
  
"Nadhani tutakuwa sawa. Bila shaka tutakosa mwendo kasi wa juu, lakini 2019 niliweza kumaliza miongoni mwa washindi wa jukwaani não Maverick [Vinales] na Vale [Valentino Rossi] wakamaliza katika nafasi za 4 na 5. Kwa hivyo sio mkondo mbaya sana kwa timu ya Yamaha, ni vile tu sio rahisi.”
  
Zarco pamoja na mwendeshaji aliyeshika nafasi ya tatu Francesco Bagnaia, wa timu ya Lenovo Ducati, wanatumainia nguvu mpya ya pikipiki zao kutoka Italia itajidhihirisha kwenye barabara za Spielberg, hatua inayotarajiwa kuwa ya kusisimua ya mashindano ya  MotoGP. 
  
Watano bora katika Mashindano ya 2021 MotoGP 2021

 
1 – Fabio Quartararo (Monster Energy Yamaha), Alam 156 
 
2 – Johann Zarco (Pramac Ducati), 122
 
3 – Francesco Bagnaia (Lenovo Ducati), 109
 
4 – Joan Mir (Suzuki Ecstar), 101
 
5 – Jack Miller (Lenovo Ducati), 100

 
 
Msimamo wa timu katika MotoGP 2021, tano bora
 
1 – Monster Energy Yamaha, alama 251 
 
2 – Lenovo Ducati, 209
 
3 – Pramac Ducati, 149
 
4 – Red Bull KTM, 145
 
5 – Suzuki Ecstar, 134


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 08/05/2021