Elaine Thomson-Hera aweka historia tena kwa ushindi mara mbili


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Michezo ya Olimpiki Tokyo 2020

23 Julai – 8 Agosti 2021

Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 ilimalizika mwishoni mwa wiki, ikahitimisha majuma mawili ya michuano kwenye michezo mbali mbali katika mji mkuu wa Japan. Katika Makala hii tunaangazia baadhi ya matokeo ya kusisimua kwenye michezo hiyo iliyofanyika kwa mara ya 32.

Mmoja wa wanariadha nyota alikuwa Mjamaica Elaine Thompson-Herah anayekimbia mbio fupi, na ambaye alifanikiwa kutetea dhahabu yake kwenye mbio za mita 200 kwa kukimbia muda wa sekunde 21.53, iliyomfanya kuwa mwanamke wa pili duniani mwenye kasi kubwa zaidi katika historia ya mbio hizo. Pia ndiye mwanamke wa kwanza katika historia kushinda dhahabu katika mbio za mita 100 na 200 kwenye Olimpiki moja. 

"Ni mshangao mkubwa kushinda dhahabu mbili kwa mara nyingine. Nimekuwa na wiki ngumu. Sikulala baada ya fainali ya mbio za mita 100," Thompson-Herah alisema.

Thompson-Herah alitumia nguvu nyingi huku akifuatwa kwa karibu na Christine Mboma wa Namibia na Mmarekani chipukizi Gabby Thomas katika mita 200, baada ya kuongoza Wajamaica wenzake Shelly-Ann Fraser-Pryce na Shericka Jackson kuzoa medali zote kwenye mbio za mita 100.

"Kusema kweli nimechoka sana," Thompson-Herah alisema. "Miguu yangu inahitaji kupumzika. Nimekimbia mbio nyingi ndani ya siku chache zilizopita, lakini nashukuru sana.”

Lakini wanaume wa Jamaica hawakuwaiga kina dada wa nchi hiyo katika kuhodhi mbio fupi, huku Rasheed Dwyer, mwakilishi pekee kwenye fainali ya mbio za mita 200 akimaliza wa saba. Na hiyo ni baada ya mwanariadha wao hodari Usain Bolt kushinda mbio za mita 100 na mita 200 kwenye michezo ya Olimpiki ya 2008, 2012 na 2016.

“Nilifikiri kwenye michezo ya Olimpiki kadhaa iliyopita tumekuwa na wanariadha Hodari,” alisema Bolt. “Kwa hivyo kwa kweli inanipa usumbufu kujua hapa ndio tulipo sasa hivi, na dunia nyingine imetuwacha nyuma. Nimevunjika moyo kwa sababu nadhani tuna vijana wenye vipaji, na swala la kuwatambua tu na watu wachukulie mazoezi kwa umuhimu mkubwa.”
 

Msimamo wa mwisho wa Medali, tano bora


1 – Marekani – Dhahabu 39 – Fedha 41 – Shaba 33 – Jumla 113
2 – China – Dhahabu 38 – Fedha 32 – Shaba 18 – Jumla 88
3 – Japan – Dhahabu 27  –  Fedha 14 – Shaba 17 – Jumla 58
4 – Uingereza – Dhahabu 22 –  Fedha 21 – Bronze 22 – Jumla 65
5 – R.O.C. (Urusi) – Dhahabu 20 – Fedha 28  – Shaba 23 – Jumla 71 

Shabikia timu yako na bashiri sasa na Betway

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway

Published: 08/11/2021