Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Ligi kuu ya Uhispania
Siku ya 1
Celta de Vigo v Atletico Madrid
Abanca-Balaídos
Jumapili, 15 Agosti 2021
Muda- 18:30
Celta Vigo itapepetana na Atletico Madrid kwenye
Ligi kuu ya Uhispania katika uwanja wa Abanca-Balaídos Agosti 15.
Celta Vigo walifungwa 3-2 na Real Betis kwenye mechi yao ya mwisho msimu wa 2020/21 iliyochezwa tarehe 22 Mei.
Matokeo hayo yalikata mtiririko wa Celta wa mechi tano bila kupoteza kwenye ligi hiyo, baada ya kushinda mechi tano mtawalia.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Pia yalikatisha mfululizo wa mechi tatu nyumbani bila kupoteza, ambapo walikuwa wameandikisha ushindi mara tatu mtawalia.
Wakati huo huo, Atletico waliwafunga Real Valwa 2-1 ugenini na waliweza kutwaa ubingwa wa Ligi katika siku ya mwisho ya msimu uliopita, mechi iliyochezwa tarehe 22 Mei.
Timu hiyo ya kampuni ya kutengeneza magodoro haijapoteza katika mechi tano zilizopita kwenye ligi baada ya kushinda nne na kutoka sare mara moja.
Atletico pia hawajapoteza ugenini katika mechi tatu za La Liga wakiwa wametoa sare moja na kushinda mara mbili.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Rodrigo de Paul, kiungo mpya wa Atletico, anatazamia kuwachezea mabingwa hao wa La Liga chini ya ukufunzi wa meneja Diego Simeone.
"Nafurahia sana kufanya kazi kwa maelekezo ya Simeone. Kwa sababu ya haiba yake kama kocha, mmoja wa walio bora,” De Paul alisema.
"Napenda soka, na naishi soka kila siku, na kuongozwa na kocha kama Simeone- kutoka nchi yangu, inanipa fahari kubwa kama mchezaji. Napenda kuwa chini ya uongozi wake kwa sababu nilikua nikimtazama akichezea timu ya taifa ya Argentina.”
Mara ya mwisho Celta na Atletico kukutana kwenye ligi ilikuwa Februari 8, 2021.
Timu hizo zilitoka sare 2-2 mtanange uliopigwa katika uwanja wa Estadio Wanda Metropolitano.
Matokeo ya mechi tano zilizopita
Mechi - 5
Celta - 0
Atletico - 2
Sare - 3
Odds bomba za kubashiri mpira wa miguu na machaguo yaliyoboreshwa zaidi, kubashiri michezo haijawahi kuwa rahisi hivi. Jiunge na Betway sasa ubashiri La Liga kwa Free Bet TSh 3,000.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway