Hakimiliki ya picha: Getty Images
MotoGP 2021- Ubingwa wa Dunia
Mkondo wa 14
San Marino and Rimini Riviera Grand Prix
Uwanja wa Misano World Marco Simoncelli
Jumapili, Septemba 19, 2021
15:00
Mwendeshaji anayeongoza mashindano ya mbio za pikipiki ya 2021
MotoGP Ubingwa wa Dunia Fabio Quartararo anatazamia kurudi kwa kishindo baada ya kupata matokeo mabaya mkondo uliopita wakati mkondo wa 14 wa mashindano hayo San Marino and Rimini Riviera Grand Prix, yatakapofanyika katika uwanja wa Misano World Circuit Marco Simoncelli Jumapili Septemba 19.
Quartararo alifanikiwa tu kushika nafasi ya nane kwenye mashindano ya Aragon Grand Prix nchini Uhispania mwishoni mwa wiki iliyopita, matokeo yaliyosababisha kupungua kwa alama ambazo amewaacha nazo wapinzani wa karibu katika msimamo zikawa 53. Mshindi alikuwa Francesco Bagnaia wa Lenovo Ducati na ndiye mpinzani anayemkaribia Quartararo (Ilikuwa mara ya kwanza kwa Mwitaliano huyo kushinda mashindano ya MotoGP, huku akifukuziwa kwa karibu na Marc Marquez).
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Bingwa wa dunia Joan Mir wa timu ya Ecstar Suzuki yuko alama nne tu nyuma. Mfaransa Quartararo bado yuko imara kileleni, lakini hakufurahishwa na namna pikipiki yake, hususan magurudumu yalivyokuwa katika mashindano ya Aragon.
“Baada ya mazoezi nilitarajia kupambana kuwa kwenye jukwaa la washindi kwa sababu nilihisi nilikuwa na kitu kizuri- magurudumu makuu kuu. Nilikuwa najisikia vizuri sana baada ya mizunguko 26 na nikaamini nitaweza,” Quartararo alisema.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Toka mwanzoni gurudumu la nyuma halikuwa linafanya kazi inavyotakiwa. Nilipunguza kasi, na kupunguza tena. Kitu pekee cha kufurahisha siku hiyo kilikuwa kupigania nafasi yangu, nilikuwa napambana, sikukata tamaa, hata kama nilikuwa kwenye nafasi ya saba, nane, au ya tisa. Nilipambana mpaka mwisho, na hilo ni jambo zuri.”
Mwendeshaji huyo wa Yamaha atatumainia kuwa atakuwa vizuri tena shindano la San Marino GP, baada ya kupata ushindi mashindano ya Doha, Ureno, Italia, (Mugello), Uholanzi na Uingereza kufikia sasa kwenye kampeni ya 2021.
Msimamo wa Waendeshaji
1 – Fabio Quartararo, Monster Energy Yamaha, alama 214
2 – Francesco Bagnaia, Lenovo Ducati, 161
3 – Joan Mir, Ecstar Suzuki, 157
4 – Johann Zarco, Pramac Ducati, 137
5 – Jack Miller, Lenovo Ducati, 129
Msimamo wa Timu
1 – Monster Energy Yamaha, alama 309
2 – Lenovo Ducati, 290
3 – Ecstar Suzuki, 225
4 – Pramac Ducati, 212
5 – Red Bull KTM, 204
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni
soka,
motorsport,
mpira wa kikapu,
rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway