Atleti yalenga kudumisha mwanzo mzuri wa LaLiga


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2021/22 LaLiga ya Uhispania 

Mechi ya 2 kati ya 38

Atletico Madrid vs Elche 

Estadio Wanda Metropolitano
Madrid, Spain
Jumapili, 22  Agosti 2021
Mechi kuanza 19:30 CAT 
 
Mabingwa watetezi Atletico Madrid wanalenga kuendeleza mwanzo wao mzuri katika msimu wa  2021/22 wa Laliga watakapowakaribisha Elche kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano jumapili.  
  
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Angel Correa
 Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
Atleti walianza kutetea taji vizuri kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Celta Vigo. Angel Correa aliendelea alipoachia msimu uliopita kwa kufunga magoli mawili yaliyowawezesha klabu hiyo ya mjini Madrid kuzoa alama zote tatu.
  
"Tulicheza vizuri sana, tukadhibiti mchezo nusu ya kwanza na kuwasababishia matatizo mengi langoni timu ambayo hucheza mpira mzuri sana," meneja wa Atletico Diego Simeone alisema.  
  
"Penalti hiyo ilibadilisha mchezo lakini tulisawazisha kwa goli la kufurahisha. Tulicheza mchezo wa kasi sana na hiyo ilinipa furaha.” 
  
Elche walimaliza msimu uliopita kwa ushindi wa mechi kadhaa na walianza msimu huu mpya kwa sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Athletico Bilbao. 
  
Lucas Boye of Elche
 Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
Atletico walishinda mechi zote mbili dhidi ya Elche msimu uliopita. Kikosi cha Simeone kilishinda 3-1 nyumbani na 1-0 ugenini.  
  

Takwimu za Atletico Madrid vs Elche:

  
Mechi zilizochezwa: 12
Atletico Madrid wakashinda: 9
Elche wakashinda: 2
Sare: 1
 

Ratiba ya Ligi kuu ya Uhispania (Laliga) wikendi ya 2: 

 
Ijumaa, Agosti 20
 
21:00 - Real Betis vs Cadiz 
 
Jumamosi, Agosti 21 
 
17:00 - Alaves vs Mallorca 
19:30 - Granada vs Valencia 
19:30 - Espanyol vs Villarreal 
22:00 - Athletic Bilbao vs FC Barcelona 
 
Jumapili, Agosti 22  
 
17:00 - Real Sociedad vs Rayo Vallecano 
19:30 - Atletico Madrid vs Elche 
22:00 - Levante vs Real Madrid 
 
Jumatatu, Agosti 23 
 
20:00 - Getafe vs Sevilla 
22:00 - Osasuna vs Celta Vigo 

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway
 

Published: 08/20/2021