Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 10
Manchester United v Manchester City
Old Trafford
Manchester, England
Sunday, 29 October 2023
Manchester United watakuwa mwenyeji wa Manchester City ugani Old Trafford Oktoba 29 katika
mechi ya ligi ambayo itakuwa ni dabi ya 191, mechi itakayo kuwa na athari kubwa katika msimu wa United.
The Red Devils wamekuwa na matokeo mseto msimu huu na kuonyesha udhaifu unaotia shaka iwapo wataweza kuibuka na ushindi dhidi ya City kama ilivyokuwa miezi kumi iliyopita walipowashinda City 2-1.
Ushindi wa 2-1 dhidi ya Sheffield United, Bramall Lane on Oktoba 21 utakuwa uliwapa motisha baada ya Diogo Dalot kufunga goli zuri la ushindi kwa vijana wa Erik ten Hag. Huu ulikuwa ni ushindi wa tano kwao msimu 2023-24.
United wanashikilia nafasi ya nane kwenye jedwali, alama sita nyuma ya majirani wao waliokwea hadi nafasi ya kwanza baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton.
Brighton, maarufu kama Seagulls wapo katika nafasi ya 7, Arsenal nafasi ya 2, Newcastle 6, Aston Villa 5 huku Liverpool wakishika nafasi ya 3 baada ya kushinda mchezo wao uliopita.
Alamy hisa picha
Ushindi wa City dhidi ya Brighton ulikuwa muhimu ikiwa unakuja baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo mikononi mwa Wolves na the Gunners kabla ya mapumziko kuelekea mechi za kimataifa.
Kwa pamoja Arsenal, timu ya Pep Guardiola imejizolea alama 21 ila inawashinda miamba hao kutoka London kwa ubora wa magoli.
Sofyan Amrabat anatarajiwa kuwajibika kwa kiwango kikubwa dhidi ya City baada ya Casemiro kupata jeraha akichezea timu ya taifa na kupelekea kukosa mechi ya ligi iliyopita. Kiungo huyo kutoka Morocco amecheza mechi mbili tu katika nafasi yake akiwa na United baada ya kuanza kama mlinzi kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Crystal Palace kutokana na majeraha mengi kwenye safu ya ulinzi.
Alamy hisa picha
Jeremy Doku amekuwa akionyesha uchezaji mzuri tangu ajiunge na City akitokea Rennes. Aliisababishia matatizo makubwa safu ya ulinzi ya Brighton na hasa pembezoni kushoto alipotoa pasi nzuri iliyosababisha goli la Julian Alvarez dakika ya saba ya mchezo. Raia huyo wa Ubelgiji alipata goli lake la kwanza akiwa na City alipofunga dhidi ya West Ham.
Rasmus Hojlund hajafanikiwa kufunga goli katika mechi ya Premier lakini amefunga magoli matatu kwenye mechi mbili za klabu bingwa ulaya. Hata hivyo, Ten Hag hana wasiwasi na hali hiyo kwani ana imani mshambuliaji huyo kutoka Denmark atapata nafasi kuonyesha uwezo wake.
"Sio tatizo. Amefanikiwa kufungia Denmark, ametupatia magoli kwenye mechi za UEFA hivyo basi atatufungia kwenye ligi pia,” alisema kocha huyo kutoka Uholanzi.
"Sina shaka na hilo. Leo amepata nafasi mbili au tatu nzuri. Wakati mwafaka ukifika matunda yake yataonekana.”
Guardiola alimsifia sana Doku ambaye alipata tuzo la mchezaji bora wa mechi dhidi ya Brighton kwa kuingiliana vizuri na kikosi chake kipya.
"Nimefurahishwa na mchango wake tangu ajiunge na sisi,” alisema Guardiola. “Hakucheza katika mechi moja au mbili baada ya mechi dhidi ya West Ham kwa sababu hajazoea kucheza mechi nyingi mfululizo.
"Ni winga mzuri. Ana uwezo mkubwa hasa anapozuia. Juhudi zake zilitupatia bao la kwanza. Huu ni mwanzo tu katika miaka mingi akiwa na timu.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Man United - 2
Man City - 3
Sare - 0
Ratiba ya mechi za ligi ya Premier mchezo wa 10:
Ijumaa, Oktoba 27
10:00pm: Crystal Palace v Tottenham Hotspur
Jumamosi, Oktoba 28
2:30pm: Chelsea v Brentford
5:00pm: Bournemouth v Burnley
5:00pm: Arsenal v Sheffield United
7:30pm: Wolverhampton Wanderers v Newcastle United
Jumapili, Oktoba 29
4:00pm: West Ham United v Everton
5:00pm: Aston Villa v Luton Town
5:00pm: Brighton & Hove Albion v Fulham
5:00pm: Liverpool v Nottingham Forest
6:30pm: Manchester United v Manchester City
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.