Reds wapania kufufua matumaini dhidi ya City


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 11

Liverpool v Manchester City

Anfield
Liverpool, England
Sunday, 16 October 2022
Kick-off is at 17h30
 
Liverpool wanapania kufikisha kikomo msururu wa mechi tano za ligi bila ushindi watakapomenyana na Manchester City kwenye mechi ya ligi ugani Anfield Jumapili Oktoba 16.
 
The Reds walipambana na City unyo kwa unyo msimu uliopita katika azma ya kushinda taji la ligi kuu kabla ya kupoteza taji hili kwa City na alama moja ila msimu huu wanaonekana kuwa katika hali ngumu.
 
Timu ya Jurgen Klopp ilipoteza 3-2 dhidi ya viongozi wa ligi Arsenal Jumapili na sasa wapo katika nafasi ya 10 kwenye jedwali bila ushindi katika mechi tatu zilizopita.

Roberto Firmino of Liverpool
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mabingwa hao wa msimu 2019/20 tayari wapo nyuma ya wapinzani wa Jumapili kwa alama 13 huku Klopp akikiri kusikitishwa na jinsi timu hiyo inavyocheza kwa sasa na kuwaasa wachezaji wake kuzidi kupambana.
 
"Tuna changamoto sasa hivi ila tumecheza vizuri dhidi ya mpinzani mzuri anayeongoza ligi na anayecheza vizuri kwa sasa. Licha ya hali yetu ya sasa na mabadiliko yaliyotokea kwenye timu yetu, juhudi zetu zimeonekana dhidi ya timu nzuri,” alisema raia huyo wa Ujerumani baada ya mechi dhidi ya the Gunners.
 
"Katika hali tuliyonayo, tumecheza na Arsenal na mechi inayofuata tunacheza dhidi ya City. Sidhani ni wakati mwafaka kujikwamua ila tutaingia uwanjani na nia ya kutafuta alama tatu na tutapambana kadri ya uwezo wetu.
 
"Hutufurahi kuwa katika hali hii na wala hatutawaza sana kuhusu mafanikio ya msimu uliopita.”
 
City waliendelea na makali yao kwa kupata ushindi mmono wa 4-0 dhidi ya Southampton Jumamosi na wanaendelea kubaki alama moja nyuma ya viongozi Arsenal.
 
Ulikuwa ushindi wa nne mfululizo kwa City katika ligi huku Erling Haaland akifunga tena na kufikisha idadi ya magoli 15 ya ligi msimu huu.

Erling Haaland
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Pep Guardiola amemsifia Haaland kwa kumsaidia kiungo Kevin De Bruyne kuimarisha mchezo wake na kuandikisha msaada wa goli wa tisa msimu huu alipomuandalia Phil Foden pasi murua dakika ya 32.
 
"Kevin ni tishio kubwa kwa kasi na maarifa aliyo nayo. Anasaidia timu pakubwa,” alisema Guardiola.
 
"Alikuwa na mchango mkubwa leo japokuwa ana uwezo wa kucheza vizuri zaidi. Tuna wachezaji wazuri kama Julian Alvarez, Phil na wengine walio na uwezo wa kupokea pasi za Kevin.”
 

Takwimu baina ya timu hizi mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Liverpool - 0
Man City - 2
Sare - 3
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 
 

Published: 10/14/2022