Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 13
Chelsea v Manchester United
Stamford Bridge
London, England
Saturday, 22 October 2022
Kick-off is at 19h30
Chelsea wanatarajia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri chini ya ukufunzi wa Graham Potter watakapocheza na Manchester United Stamford Bridge Jumamosi Oktoba 22.
Potter alichukua mikoba ya Thomas Tuchel Septemba 8 na amesaidia Chelsea kushinda mechi nne za ligi mfululizo huku wakikosa kuruhusu goli lolote katika michezo miwili.
Hata hivyo, timu hiyo kutoka London haijakuwa na matokeo mazuri dhidi ya Red Devils hivi majuzi huku
mechi nne za mwisho baina yao zikiishia sare.
Ushindi wao wa mwisho dhidi ya United katika ligi ulikuwa mnamo Novemba 5 2017 kupitia goli moja lililofungwa na Alvaro Morata.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mason Mount alifunga magoli mawili Jumapili dhidi ya Aston Villa, Chelsea walipopata ushindi wa 2-0 ugani Villa Park. Kiungo huyo alisifiwa sana na kocha wake kama alivyomsifia mlinda lango Kepa.
"Nimefurahishwa na matokeo kwa sababu tumepambana sana kwenye mchezo huo,” alisema. Aston Villa walitubana sana hasa kipindi cha kwanza.
"Tulianza mechi vizuri lakini tukapoteza mwelekeo sehemu ya pili ya kipindi cha kwanza. Mlinda lango wetu Kepa alituokoa nyakati hizo. Nahisi kipindi cha pili tulicheza vizuri na kuwadhibiti wapinzani wetu.
"Nimefurahishwa na alama tatu tulizopata, kucheza mechi bila kuruhusu goli na vile vile na uchezaji wa Mount na Kepa haswa. Bidii yao imetuwezesha kupata ushindi huu.”
United hawajapoteza mechi ya ligi tangu walipochapwa 6-3 na majirani wao Manchester City huku Erik Ten Hag akipata sare yake kwanza Jumapili dhidi ya Newcastle tangu alipochukua mikoba Old Trafford.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ten Hag alihisi walistahili alama tatu kwenye mechi hiyo ukizingatia uchezaji wao licha ya mchezaji wa Newcastle Joelinton kupiga chuma mara mbili.
"Tunasikitika kwa sababu hatukupata ushindi licha ya uchezaji wetu mzuri,” alisema raia huyo wa Uholanzi. “Tuliwadhibiti vizuri, hatukuruhusu goli na tulikuwa na mchezo mzuri kwa ujumla.
"Nahisi tulicheza vizuri sana hasa katika kipindi cha pili tofauti na hali ilivyokuwa kipindi cha cha kwanza ambapo hatukuwa na uelewano mzuri. Newcastle ni timu inayotumia nguvu sana lakini tuliwamudu. Mwishowe hatukupata ushindi ambao nahisi tulistahili.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi
Mechi - 5
Chelsea - 0
Man United - 1
Sare - 4
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.